27 February 2013

Basi la Simba Mtoto laungua moto, abiria 60 wanusurikaNa Steven William, Muheza

ABIRIA 60 waliokuwa wakisafiri na basi la Simba Mtoto kutoka Dar es Salaam kwenda Tanga, wamenusurika kufa baada ya basi
hilo kuungua moto wakati abiria hao wakiwa ndani ya basi.

Basi hilo lina namba za usajili T 147 BWR ambapo ajali hiyo imetokea juzi usiku kwenye Kijiji cha Mkanyageni, Wilaya
ya Muheza, mkoani Tanga.

Akizungumza na gazeti hili, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Costantine Massawe, alisema chanzo cha ajaloi hiyo ni shoti ya
umeme hivyo abiria walianza kupiga kelele ya kuomba msaada.

“Hakuna abiria aliyekufa katika ajali hii, wengine wamejeruhiwa wakati wakiminyana kutoka ndani ya basi ili kuokoa maisha yao
na kuacha mabegi ambayo yaliungua,” alisema.

No comments:

Post a Comment