11 February 2013

Familia yaililia serikali kuokoa mali zao



Na Mariam Mziwanda

FAMILIA ya marehemu Maulid Salum imeendelea na kilio cha kuomba serikali kuwasaidia kuokoa mali zao kutokana na tatizo la kutokufunguliwa kwa mirathi ili watoto waweze kurudi shule.


Akizungumza jijini Dar es salaam jana mtoto wa marehemu Maulid Seif Juma (18), ameeleza kusikitishwa na hali iliyopo sasa katika familia hiyo, ambapo hata maisha yao yapo hatarini kutokana na kudai mirathi hiyo iliyopelekea ugomvi mkubwa na baadhi yao kuapizana kwa kushika msaafu bila kupata ufumbuzi.

"Mimi naomba kama kweli serikali ipo na ipo kwa ajili ya watu kama sisi tusio na makosa itusaidie na kama hamna njia ya kutusaidia mimi nipo tayari kufa lakini sio kuona mali za baba yangu zinateketea tena huku mimi na ndugu zangu tukidhulumiwa ni bora hata nife,"alisema

Seif aliyasema hayo katika ugomvi wa familai hiyo uliotokea kijitonyama wanakoishi mara baada ya kushinikizwa kusaini hati ya kuthaminishwa kwa mali zao ambayo haikuwa kwa jina halali la baba yake Maulid Salum badala yake lilikuja kwa jina la Salum Salum.

Alisema kuwa mbali na hatua hiyo awali alipigiwa simu akiwa Uganda masomoni na kutakiwa aje kusaini hati ya kuuzwa moja ya gari ya baba yake na alipofika nchini akakataa hali iliyozua chuki baina yake na familai hiyo na kutokuruidishwa tena shule.

Alisema baada ya kubaini hali hiyo alimueleza mama yake mzazi ili kupata ufumbuzi hatua ambayo ilipelekea kupelekwa polisi na kwa tuhuma zisizo za kweli na baada ya kupata dhamana msaada mkubwa wa maisha yake yamekuwa yakitokana na  majirani.

"Sisi tumezaliwa watatu wa mama mmoja ambapo mama yetu aliachika na baba akaza tena Msumbiji watoto wawili hivyo tupo watano lakini nashangaa dada yetu mkubwa ambaye yupo chuo hashirikishwi anaambiwa si mtoto halali dini hamruhusu kuruthi mali mama aliolewa na mimba nang'ang'anizwa mimi tu kusaini kila kitu sisi tunamjua ni dada yetu kama kumkataa angemkataa baba akiwa hai"

Aliongeza kuwa mbali na mgogoro huo wanachohitaji zaidi kutoka kwa Serikali ni kuona baadhi ya ndugu wa baba yao wanaridhia kufunguliwa mirathi ili wwaweze kuwa wamiliki halali wa mali za baba yao na kuweza kujilipia ada kwenda shule.

"Toka baba kufa ni miaka mitatu sasa mali zote anamiliki shangazi ambaye hataki kusikia habari ya mirathi juzi dada alikwenda haki za binadamu akapatiwa nakala ya barua ili familia ifungue mirathi baada ya hiyo barua mimi nilifuatwa na mjumbe na alinitukana na kuniambia maneno mazito nikiwa sebuleni, ambapo kwa sasa ndipo ninapolala mbali na baba yangu kuacha nyumba kubwa,"alisema

Kwa upande wa mjumbe huyo ambaye jina lake halikupatikana alikana kumtukana mtoto huyo na kueleza kuwa awali hakujua upana wa mgogoro huo na alifuatwa na shangazi akimtaka kutafuta ufumbuzi juu ya mali za familai hiyo ambazo zinatakiwa kufunguliwa mirathi na watoto hao.

Alisema alipofika katika nyumba hiyo usiku alizungumza na mtoto huyo na kumueleza malalamiko ya kumpiga bibi yake kwa chupa kwa sababu ya kudai mirathi ambapo naye alikata.


Naye mama mzazi wa watoto hao Husna Yauo aliiomba serikali imsaidie ili watoto wao waweze kupata haki zao za msingi kwani yeye alivyopewa talaka aliacha mali zote zikiwemo nyumba, gari na yadi moja ya magari akiamini kuwa ana watoto hivyo anavitaka vyombo vya sheria visimamia haki za watoto hao.



No comments:

Post a Comment