11 February 2013
Apendekeza sheria iandikwe kwa Kiswahili
Na Timothy Itembe, Tarime
KATIBU Tawala wa Wilaya ya Tarime Bw. Erenest Kabohola amewataka Mahakimu nchini katika mchakato wa kupata katiba mpya wapendekeze sheria za nchi ziandikwe kwa lugha ya Kiswahili ili kuleta uwelewa mpana kwa mwananchi asiyefahamu lugha ya kingereza.
Kabohola alisema kuwa Watanzania waliowengi wanatumia Lugha ya kiswahili kwahali hiyo sheria inapotafsiriwa kwa lugha rahisi inampa mtumiaji uelewa mpana wa kesi inavyoendelea kuliko ile ya Kingereza," alisema.
Kabohola alisema kuwa Watanzania walio wengi hawazijui sheria kwakuwa zimeandikwa kwa lugha ya kingereza nakwamba endapo sheria zikiandikwa kwa Kiswahili zitamwezesha mwananchi kuzielewa hivyo zitasaidia kupunguza uhalifu kwakuwa watu wengi wamekuwa wakifanya uhalifu kwakuwa hawafahamu sheria .
“kwakuwa sasa ni kipindi cha mchakato wa kupata katiba mpya nawashauri mahakimu mnapotoa naoni yenu pendekezeni sheria ziandikwe kwa Kiswahili, watu wanafanya matukio mabaya kwakuwa hawaifahamu sheria waliowengi hawafahamu lugha ya kingereza histoshe sisi si waingereza sheria ziandikwe kwa Kiswahili kila mtu azijue” alisema kabohola.
Akiongea katika sherehe za mahazimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika ndani ya mahakama ya Wilaya ya Tarime.
Kabohola ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alisema kuwa imefika wakati sasa sheria za nchi zitungwe na kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili na siyo kingereza.
Kabohola alisema kuwa lugha ya kingereza inawapa wakati mgumu wananchi wenye kesi zao mahakamani kushindwa kuelewa kilichoandikwa kwenye karatasi zikiwemo hukumu la lufaa ambazo zimekuwa zikiandikwa kwa kingereza.
Pia Kabohola aliwataka watumishi kufuata misingi ya utawala bora nakwamba endapo ikizingatiwa italeta huduma iliyobora kwasasabu lengo ni kutumikia wananchi hivyo hata kesi zinazochelewa kutolewa uamuzi zitatolewa uamuzi kwakuwa misingi ya utawala bora imefuatwa.
Aliongeza kuwa nchi sasa imekumbwa na vurugu zinazohatalisha amani ya nchi nakwamba lengo kubwa la utawala wa kisheria ni kuleta amani na utulivu wa nchi hivyo sheria itumike bila ubaguzi wowote.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tarime Yusto Ruboroga alisema kuwa kutokuwepo kwa utawala wa kuzingatia sheria ndiyo matarajio ya watu kujichukulia sheria mkononi hivyo akawaasa viongozi kuweka masahi ya nchi mbele bila kujali maslahi ya mtu aliyemwajiri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment