27 February 2013

Dkt. Nagu awashukia walimu


Na Peter Ringi, Hanang

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni mbunge wa Hanang’, mkoani Manyara, Dkt. Mary Nagu, amesema kushuka kwa kiwango cha ufaulu nchini
kinachangiwa na walimu wasio na wito.


Dkt. Nagu aliyasema hayo mwishoni mwa wiki  jimboni humo katika kikao chake na wakuu wa  shule za msingi na sekondari, ambacho kilikuwa na lengo la kubaini tatizo hilo.

“Wote mlioomba kazi ya ualimu ni wazi mna wito, wale wasio
na wito ni vyema wakatafuta kazi nyingine badala ya kuendelea kubaki kwenye ajira wasiyoimudu.

“Lazima walimu waone fahali ya kufaulisha watoto, yapo madai ambayo wanaidai Serikali lakini si kigezo cha kuvunja wito wao,” alisema Dkt. Nagu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Bw. Filex Mabula, alisema wamejipanga kuhakikisha ifikapo Mei mwaka huu, madeni ya walimu yatakuwa yamepunguzwa au kwisha kabisa.

No comments:

Post a Comment