07 February 2013

Dawa ya waendesha bodaboda yapikwa

Na Grace Ndossa

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imesema kuwa kwa sasa wako kwenye hatua za kuchambua makampuni yaliyoomba tenda ya kukamata pikipiki na magari yanayoegeshwa kiholela mjini.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Ofisa habari wa Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu alipokuwa anazungumza  na gazeti hili ofisini kwake.

Alisema kuwa mwisho wa kupokea barua za maombi kwa  kampuni hizo ilikuwa ni jumatatu wiki hii na kwa sasa wameshaanza kuchambua kampuni ipi bora inayofaa kwa kazi hiyo.

"Tulipiga marufu pikipiki kuingia mjini lakini  bado zimeendelea kuongezeka kwa kiasi kikubwa hivyo kampuni itakayochagulkiwa kufanya kazi hiyo itatusaidia kupunguza ili wimbi la pikipiki kuingia mjini na magari yanayopaki kiholela,"alisema Bi. Tabu.

Alisema kuwa Pikipiki ziliruhusiwa kufanya kazi zake nje ya mji lakini mpaka sasa hivi zimeongezeka kwa kasi sana  na zinapaki kila sehemu hali ambayo siyo nzuri.

Hata hivyo alisema pikipiki nyingi zinazpoingia mjini hawafuati taratibu na sherioa za barabrani kitu kinachopelekea kuendesha vibaya na wakati mwingine kusababisha ajali .

Mwishoni mwa mwaka jana Jeshi la polisi kwa kushirikina na Manispaa ya Ilala walipiga marufuku pikioiki kuingia mjini kwani mara nyingi zinatumika kufanya uhalifu na kusababishja ajali zisizotarajiwa.

1 comment:

  1. Kukamata pikipiki pia mnatoa tenda? Itafika wakati mpaka kazi za polisi, jeshi, Takukuru na kadhalika mtaalika tenda

    ReplyDelete