07 February 2013

Rehema Maigala na Christina Mokimirya



WAMILIKI wa majengo marefu wametakiwa kuweka ving'amuzi katika majengo yao ili kupunguza ajali za moto zinazotokea mara kwa mara.


Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam Kamishna Mkuu wa kikosi cha zimamoto Pius Nyambacha alisema ving'amuzi vitasaidia kupunguza ajali za moto.

Alisema kuwa si katika majengo tu bali hata katika nyumba binafsi wamiliki wanatakiwa kununua ving'amuzi hivyo ili kuondoa janga la moto ambalo huwapa watu umasikini.

"Mara nyingi tukikagua majengo huwa huwa tunatoa ushauri kuwa ni lazima kila jengo liwe na ving'amuzi ili kuepukana na ajali ya moto"alisema

Aliongeza kuwa ving'amuzi vinasaidia kujua haraka ajali ya moto kama inatokea hivyo tahadhari ya haraka inaweza kuchukuliwa na kuudhiti moto usiendelee kuenea .

Alisema kuwa majengo yamejengwa ni marefu na ni mazuri ambayo yanapendezesha mji lakini cha ajabu hawafati kanuni tunazowapa wakati tunapokwenda kuwakagua.

Hata hivyo alisema katika teknolojia ya leo na uzuri wa majengo yanatakiwa kuwekwa vifaa ambavyo dalili za moto zikianza unatakiwa moto kujizima wenyewe.

Aidha alisema kuwa katika majengo yenye maghorofa zaidi ya nne yawe na ngazi za dharula ambao utasaidia watu kutumia pindi inapotokea janga la moto.

Alisema pamoja na kazi za uokoaji na zimamoto zinazofanywa na jeshi hilo sasa wameona wajikite zaidi katika kuelimisha jamii juu ya kujikinga na majanga ya moto kwa kutumia ving'amuzi hivyo.

Vile vile Kamishina Nyambacha alisema kuwa kwa sasa wapo katika mchakato wa kukagua majengo ambayo hayana vidhibiti moto ili hatua kali dhidi yao iweze kuchukuliwa.

No comments:

Post a Comment