07 February 2013

Wananchi Ilala washauriwa kuweka taratibu za usafi



Na Rehema Maigala

MEYA wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa ameishauri jamii kuwa utaratiu wa kufanya usafi katika maeneo wanayoishi na ya biashara kwa kukata miti na kulima maji ili kuwa na mazingira masafi yenye kuvutia.


Hayo alisema jana alipokuwa anazungumza na gazeti hili kuhusu suala la usafi katika manispaa ya Ilala.

Alisema kuwa kila mtu anawajibu wa kulipa ada ya takataka katika eneo analoishi na sehemu ya kufanyia kazi ili kukaa katika mazingira yaliyo safi na salama kwa ajili ya afya ya kwa pamoja.

Alisema suala la usafi katika manispaa ya Ilala kwa hivi sasa linaenda vizuri ni baada ya viongozi wa Serikali ya mitaa kukaa pamoja na wananchi wake na kuongelea suala zima la usafi.

"Kuna usemi usemao kuwa usafi huficha umasiki hivyo ni wajibu wa kila mtu kuhimiza usafi ili Manispaa ya Ilala iendelee kuwa safi wakati wote na iwe Manispaa ya kuigwa katika jiji la Dar es Salaam," alisema Silaa.

Aliongeza kuwa Manispaa ya Ilala ina mpango wa usafi ambao ulianza 2010 ambapo hadi sasa unaendelea vizuri na zipo baadhi ya taasisi ambazo zimejitokeza ili kuboresha mpango huo.

Aidha alisema mwananchi yeyote akifuatwa na mkusanya ushuru kwa ajili ya usafi asisite kutoa fedha kwani fedha hizo ndizo zinazosaidia kuiweka Ilala katika mazingira safi kwa kuboresha usafi .

Hata hivyo Silaa aliwataka viongozi wa mitaa wao ndio wawe chachu ya usafi huku wakifuatiwa na ngazi za juu.

"Tukianza ngazi ya chini kuhusu suala la usafi hata ngazi za juu itakuwa ni rahisi kuwakaribia katika suala zima la usafi,"alisema Silaa.

No comments:

Post a Comment