11 February 2013

CCM yavuna wanachama 68 Tarime

Na Timoth Itembe,Tarime

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Tarime Mkoani Mara kimepokea wananchama wapya
zaidi ya 68 wakati wa maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa chama hicho Februali 5
ambayo yanaadhimishwa   kila mwaka.

Wanachama hao wapya walipokelewa ndani ya chama hicho pamoja na  kukabidhiwa kadi za
kujiunga na chama na Mjumbe wa NEC Wilaya Tarime Bw   Chirstopher Mwita Ghachuma
Februaly,03,2013 katika viwanja vya Sabasaba mjini hapa.

Akiwapokea wananchachama hao wapya sanjari na kuwakabidhi kadi za uwananchama Bw
Ghachuma alisema chama chake kimekuwa kikishutumiwa kuwa kimeshindwa kuwapelekea
wananchi maendeleo badala yake kimekuwa kikiwanyanyasa wanachi jambo ambalo alisema
kuwa sasa wamejipanga kuondoa makosa yaliyo kuwepo ili kurudisha heshima ya chama
kwa wananchi.

''Wananchi wamekuwa wakilalamikia chama kuto peleka maendeleo kwao jambo ambalo
tumejipanga kuondoa makosa yaliyo kuwepo sanjari na kuwaondoa watendaji ambao
walikuwa hawawajibiki ipasavyo na kuweka safu mpya ambayo itafanya yale ambayo
serikali inasema''alisema Bw Ghachuma.

Waliojiunga na chama hicho ni pamoja na Amina Kata,Devvi Buhembo,Ester Chacha,Ever
Juma,Gressi Nzoba,Juma Chacha,Neema Boniphase wengine ni pamoja na Nyamohanga
Giroma,Stella Edwini,Stephano Mororo na Zainabi Ndele ambao walipokea kadi kwaniaba
ya wenzao.

Mmoja wa wanachama hao Bw Juma Chacha amesema kuwa ameamua kujiunga na CCM kwa
kupima utekelezaji wa shuguli za miradi ya maendeleo kwa wananchi ambazo
zimetekelezwa kwa asilimia kubwa hususani kwa Wilaya Tarime kwa kulima na kuzibua
Barabara.

Kwa upande wake Bi' Neema Boniphase  amesema kuwa ameamua kujiunga na CCM kwakuwa
amepima sera za vyama vingine vya upinzani na kugundua kuwa hawana sera bali sera
yao nimatusi na kujigamba majukwaani bila utekeleza aliongeza na kusema.

Kwa upande wake kaimu katibu CCM Wilaya Tarime Bw Denisi Zacharia amesema kuwa
Wanchi wasipime chama kwa mapungufu tu kwani hakuna taasisi ambayo itafanya mazuri
tu kwa kuzingatia kuwa waliowengi hawajiungi kwaniaya kusaidia bali kwa lengo la
masilahi binafsi ambapo alionngeza kuwa Chama kimejipanga kuwatekelezea wananchi
miradi ya maendeleo.

Aidha Bw Zacharia Amewataka wananchi kujiunga na chama chake kwa kuwa kinatimiza
irani ya uchaguzi kwa kuwatekelezea wananchi maendeleo sanjari na kudumisha AMANI
kwa Wananchi wake jambo ambalo linasababisha kuwepo na maendeleo. 

No comments:

Post a Comment