21 January 2013

Wafanyabiashara wasiotumia mashine za kieletroniki kuchukuliwa hatua

Na Severin Blasio,Morogoro

MALAKA ya mapato Tanzania (TRA) itawachukulia hatua wafanyabiashara  waliosajiliwa
kwenye ongezeko la thaman (VAT) watakaobainika kutotumia  mashine za kielektroniki
zinazotoa risiti  kwenye biashara zao.


Hatua hizo ni pmoja na  kutozwa faini  kati ya shilingi milioni moja hadi tatu,ama
kufungiwa biashara zao.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa  Naibu Kamishna Idara ya Kodi za ndani
wa TRA Makao Makuu, Bi.Generose Bateyunga wakati amesema  mamlaka hiyo itafanya
ukaguzi wa kushtukiza kwa baadhi ya wafanyabiashara mkoani hapa ili
kuwabaini wanaokwepa kutumia mashine hizo.

Kamishina huyo ambaye aliambatana na Meneja wa TRA mkoani   Morogoro Bw.Hakimu
Kimungu na Maafisa wengine  alisema, kwa Mfanyabiashara aliyesajiriwa na VAT atakuwa
amefanyakosa kutotumia  mashine hizo na kwamba chini ya sheri  ya ongezeko la
thamani, risiti  moja faini yake  ni kuanzia milioni moja hadi tatu.

Bi. Bateyunga alisema mbali na kulipa faini, TRA inao uwezo wa kuifungia biashara
yake ikiwa atakuwa ni mteja sugu ambaye amekuwa ukikutwa na makosa hayo mara kwa
mara.

Aliwataka Wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa kutumia mashine hizo, na kwamba
zinamanufaa kwao ikiwa ni pamoja na kujua hali halisi ya mauzo ya bishara zao na
kutokuibiwa.

Kwa Upande wake Meneja wa TRA Mkoa wa Morogoro Bw.Kimungu aliwataka wananchi kuomba
risiti mara wanaponunua bidhaa, nakwamba tayari wanakuwa wamelipia kodi, hivyo
wanapoacha wananufaisha wafanyabiashara badala ya serikali.

Pia aliwataka kusoma risiti wanazoandikiwa ikiwa zinafanana na fedha halizi
walizotoa, na kwamba ikiwa zinamapungufu wahoji ama watoe taarifa kwenye mamalaka
hiyo, ili watu hao wachukuliwe hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment