21 January 2013

Ridhiwani: Nakerwa na ushabiki wa siasa vyuoni



Na Charles Mwakipesile, Mbeya

MJUMBE wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (NEC), Bw. Ridhiwani Kikwete, amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa Vyuo Vikuu mkoani Mbeya kujiingiza katika ushabiki wa kisiasa.


Bw. Kikwete aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifungua kongamano la wanafunzi wa Vyuo Vikuu ambao ni wanachama wa CCM mkoani Mbeya.

Alisema baadhi ya wanafunzi ambao ni wanachama wa CCM, wanadaiwa kunyang'anywa vitambulisho na viongozi hao waanapokwenda kushiriki mikutano ya chama hicho.

Aliongeza kuwa, kama viongozi hao wanataka kuingia katika ushambiki wa kisiasa, wanapaswa kuondoka katika nafasi hizo
na kutangaza rasmi vyama wanavyotaka viungwe mkono.

“Nimesikitishwa sana kusikia kuna baadhi ya wanafunzi wa chumo cha (jina tunalo), wamepokonywa vitammbulisho vyao nje ya chuo walipokuwa wanakuja kwenye mkutano huu.

“Utaratibu huu si sahihi na wamefanyiwa kitendo hiki katika muda ambao si wa masomo unaomruhusu mwanafunzi kufanya jambo lolote atakalo likiwemo la kisiasa,” alisema Bw. Kikwete.

Alisema wasomi waliooko vyuoni ni vyema wakawa huru kushiriki kwenye siasa katika muda ambao hauharibu masomo wala taratibu za vyuo ili waweze kukijua chama chao, kujiandaa kuwa viongozi wa chama na Serikali.

Bw. Kikwete alisema, Vyuo Vikuu nchini vinatengeneza viongozi wa kesho hivyo ni vyema wanafunzi wakasoma kwa bidii ili waweze kujiandaa kuwa viongozi wa chama na Serikali baada ya kuhitimu.

Aliongeza kuwa, si haki kwa wanachama wa CCM Mkoa wa Vyuo Vikuu kunyanyaswa na watawala wa vyuo husika wenye malengo yao ili kufanikisha matakwa ya watu wengine.

“Jambo la msingi mnapaswa kuwa na mshikamano thabiti ambao utasaidia kupata ushindi wa kishindo katika chaguzi za 2014 na  mwaka 2015...kwani vijana ndio wenye nafasi kubwa ya kuhakikisha ushindi unapatikana,” alisema.

Akizungumzia madai ya kunyanyaswa wanafunzi wa Vyuo Vikuu mkoani humo ambao ni wanachama wa CCM, Makamu Mkuu wa Chuo Mikuu Teofilo Kisanji, Profesa Tuli Kasimoto, alisema ni makosa kuwakataza wasishiriki siasa wakiwa nje ya chuo.

Alisema ndani ya chuo hakutakiwi siasa za chama chochote wala kuvaa sare na ikibainika, mamlaka inayosimamia vyuo vikuu inaweza kukifungia chuo kilichoruhusu siasa ndani ya chuo.


5 comments:

  1. KAMA UNAKERWA MWELEZE BABA YAKO NA SIYO SISI, MBONA HUKERWI NA....

    ReplyDelete
  2. so wewe unatakaje. unadhani unawezaje kumtenganisha mwanafunzi anaesoma political science na politics acha ushamba RIDHIWANI.

    ReplyDelete
  3. WEE UNAONGEA NINI DOGO LAKINI HIVI UKO SIRIAZ. SI UMUUNGE MAMA YAKO MKONO KTK MBIO ZAKE ZA KUMKOMBOA MWANAMKE? SIASA HUIJUI HUIWEZI SO TUACHIE SISI. YAANI LIKE FATHER LIKE SON

    ReplyDelete
  4. WAUMINI WA JAMII FORUM MUWE NA ADABU NDIO MULICHANGIA UTAFITI WA PEW CENTRE UNAOITUKANA TANZANIA KUWA NI WAVIVU WA KUFIKIRI WAMESHINDWA KUSUGUA BONGO ZAO HATA MASUALA MADOGO ASILIMIA 93 NI WASHIRIKINA WAKATI WENZAO WAKIONGOZA KWENYE ICT KWENYE SOKO LA AJIRA AFRIKA YA MASHARIKI MUTISHIA KUPIGA RANGI VIATU BADILIKENI

    ReplyDelete
  5. HIVI BILA YA KUFANYA SIASA VYUONI TUNGEPATA WAPI MAWAZO YA KULIKOMBOA BARA LA AFRIKA, UDSM PALE TAZAMA WASOMI WENGI WA BARA HILI NA VIONGOZI WA KISIASA WALIPITIA, MAKERER PALE UGANDA, HUYU RIDH AMELEWA MADARAKA YA BABA YAKE SUBIRI MZEE WAKE ATOKE TUNAMPOTEZA KABISA KATIKA ULIMWENGU WA SIASA

    ReplyDelete