21 January 2013

Ugonjwa unaomsumbua DCI Manumba kuwekwa hadharani


Na Stella Aron

UONGOZI wa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, leo unatarajia kueleza umma ugonjwa unaosumbua Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini, DCI Robert Manumba.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Tiba hospitalini hapo, Dkt. Jaffer Dharsee, alisema taarifa kamili za ugonjwa unaomsumbua Bw. Manumba zitatolewa leo.

Alisema Bw. Manumba ni kiongozi mkubwa ambaye umma unataka kujua ugonjwa unaomsumbua lakini uongozi wa hospitali hiyo ulishindwa kutoa taarifa kutokana na baadhi ya vipimo kuchukua muda mrefu hadi kupata matokeo kamili.

Hata hivyo, taarifa zaidi zilizopatikana hospitalini hapo zinadai kuwa, hali ya Bw. Kanumba bado hairidhishi na anaendelea
kupumulia mashine katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Baadhi ya viongozi wa Serikali, jana waliendelea kujitokeza kwa wingi ili kumjulia hali.

No comments:

Post a Comment