16 January 2013

Rais Kikwete awahakikishia ulinzi Mabalozi
Na Kassim Mahege

RAIS Jakaya Kikwete, amesema Tanzania itaendelea kuimarisha ulinzi kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini pamoja
na kuzikabili changamoto zilizojitokeza mwaka 2012.


Alisema Serikali ipo makini kuhakikisha hakuna mtu ambaye atahatarisha amani na utulivu uliopo ili nchi iweze kupiga hatua
kubwa ya maendeleo, kukuza uchumi wa jamii na Taifa.

Rais Kikwete aliyasema hayo Ikulu, Dar es Salaam juzi katika
hafla fupi ya kuukabirisha mwaka mpya iliyoshirikisha mabalozi
mbalimbali ambao wanaziwakilisha nchi zao nchini.

“Mwaka huu, Serikali imejipanga kupiga hatua kubwa zaidi ya maendeleo katika sekta ya madini, kilimo na uwekezaji bishara
ili kuongeza kasi ya ukuaji uchumi.

“Pia tunaendelea na mchakato wa kukamilisha Vitambulisho vya Taifa ili kila Mtanzania aweze kuwa nacho, naomba ushirikiano
wenu kwa Serikali uendelee ili Taifa liweze kutimiza wajibu
wake kwa Watanzania wote,” alisema Rais Kikwete.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Mabalozi ambao wanaziwakilisha nchi zao nchini, Balozi Juma Mpango, aliimpongeza Serikali kwa jitihada kubwa inazofanya ili kuharakisha maendeleo ya sekta mbalimbali, kuimarisha ulinzi na kulinda amani iliyopo.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, alisema mwaka huu Serikali imedhamiria kuitangaza nchi kimataifa katika mambo mbalimbali.

“Mwaka huu tutateuwa Mabalozi wa heshima wasiopunguwa
sita ili waweze kuitangaza nchi yetu kimataifa ili kutangaza
vivutio vilivyopo katika sekta ya utalii, fursa za uwezekaji
pamoja na biashara,” alisema Bw. Membe.

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja na Mataifa (UN), Dkt. Asha-Rose Migiro, alisema mwaka 2012 Tanzania ilifanya kazi
kubwa ya kutatua migogoro ukiwemo ule wa Madagasca, Malawi
hivyo mwaaka huu, imejipanga kuimarisha amani.

No comments:

Post a Comment