28 January 2013

Radi yawajeruhi mama,watoto


Na Cresensia Kapinga,Songea

MWANAMKE mmoja Zainabu Ally (33) na wanawe wawili,Ally Khamisi (5) na Hawa Nigange (4)wote wakazi wa kijiji cha Rwinga nje kidogo ya mji wa Namtumbo mkoani Ruvuma wamejeruhiwa vibaya kwa radi nje ya nyumba yao wakati walipokuwa wakila chakula.


Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Mrakibu mwandamizi wa Polisi Bw. Gorge Chiposi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa familia hiyo ilikumbwa na mkasa wakati walipokuwa wanakula nje ya nyumba yao baada ya kutoka shamba.

Kaimu Kamanda Chiposi alisema kuwa mvua kubwa ya upepo ilinyesha ghafla ikiwa imeambatana na upepo pamoja na radi ambayo iliwasababishia majeraha sehemu mbalimbali za mihili yao.

Alifafanua kuwa, Bi.Zainabu ambaye ni mama mzazi wa watoto hao alipigwa na radi na kusababisha miguu yote miwili kupooza ,Mtoto Ally radi ilimbabua maeneo ya paja la kushoto,tumboni na kwenye makalio yake na mtoto Hawa alibabuliwa na radi mikononi na tumboni.

Alisema kuwa majeruhi wote walikimbizwa katika hospitali ya serikali ya Wilaya ya Namtumbo ambako wanaendelea kupata matibabu na hali zao bado sio nzuri hata hivyo mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali mkoani humo zimeharibu miundombinu ya barabara na kusababisha usafiri kuwa mgumu.

Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Songea wamejikuta wakikosa huduma za mitandao ya E-mail (barua pepe  ambayo imesababisha huduma za ATM za taasisi za kifedha zilizopo ndani ya manispaa ya Songea na barua pepe kutofanya kazi tangu juzi kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na radi.kuarubu miundombinu na mawasiliano.No comments:

Post a Comment