18 January 2013

Nchemba ahofia ajira za wabunge CHADEMA


Na Benedict Kaguo

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Bara, Bw. Mwigulu Nchemba, amefichua siri ya kutoyaweka bayana majina ya wabunge saba
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walioomba kujiunga na chama chao.


Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Bw. Nchemba alisema hali hiyo inatokana na ukweli kwamba, kama majina hayo yatawekwa hadharani, wabunge hao wanaweza kufukuzwa uanachama ila wakati ukifika watatajwa.

Bw. Nchimba aliyasema hayo kutoa ufafanuzi wa taarifa alizotoa hivi karibuni kuwa wabunge saba wa CHADEMA waliiomba kujiunga na CCM ambapo hali hiyo iliacha maswali mengi
kwa wananchi kutaka kuwafahamu wabunge hao.

“Idadi hii ya wabunge bila kutia shaka wako saba...miongoni mwao watano wanatoka kwenye majimbo, wawili Viti Maalumu ambao wameomba wasitajwe majina wakihofia kupoteza nafasi walizonazo kwa sasa,” alisema Bw. Nchemba.

Aliongeza kuwa, mbunge mmoja wapo wa majimbo anatokea mikoa ya Kanda ya Kaskazini ambapo sababu kubwa ya kutaka kuhamia CCM ni kutokana na mgogoro ulioko ndani ya CHADEMA na kusababisha baadhi ya wanachama kufukuzwa.

“Muda ukifika majina ya wabunge hawa nitayaweka hadharani na sisi tutawapa nafasi ya kugombea majimbo hayo kwa tiketi ya CCM, chama chetu kitaendelea kuwa kinara wa demokrasia nchini kwa kukubadili kubadilika ili kuendana na matakwa ya wananchi,” alisema.

1 comment:

  1. KAMA KWELI WEWE MWANAUME UNAJIAMINI SI UWATAJE NA KAME MWANAMKE UNAYEVAA SURUALI USIWATAJE MAANA UMBEA NDIO KAZI YA WANAWAKE SASA HATA KAMA KWENYE SIASA UNALETA UMBEA HIYO NAFASI IMEKUSHINDA BORA URUDI NDAGO UKALIME ALZETI AU UKAE KIMYA KAMA MZEE WAKO KINANA KWASABABU SIFA ULIZOSIFIWA NA KIKWETE NDIZO ZINAZOKUARIBU ULIONA WAPI DIGITALI ZIKARUDI KUWA ANALOGIA AU ULIONA WAPI MATAPISHI ULIYOTAPIKA UKAYALA TENA KAMA CHAKULA ccm NI MATAPISHI HAKUNA ANAYEYAHITAJI NAKUSHAURI DESIGN PROPAGANDA NYINGINE HIYO IMESHINDWA GAMBA.

    ReplyDelete