15 January 2013

Mbaroni akidaiwa kumbaka, kumlawiti mzazi mwenzake


Na Jamillah Daffo, Babati

JESHI la Polisi mkoani Manyara, linamshikiliwa mkazi wa Kijiji cha Gijachameda, Wilaya ya Babati, Bw. John Barandi (35), kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mzazi mwenzake Mwanaisha Iddi
(25), baada ya kumbaka na kumlawiti.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Akili Mpwapwa, alisema tukio hilo limetokea Januari 10 mwaka huu, saa 11 jioni, eneo la Mrara wilayani humo.

Alisema siku ya tukio, mtuhumiwa akiwa mjini Babati alimpigia simu mzazi mwenzake ambaye inadaiwa walizaa naye watoto wawili ili wakutane na kwenda kufanya mapenzi.

“Marehemu alikwenda kwa mzazi mwenzake na kwenda kufanya naye mapenzi katika korongo la maji lilipo Mrara, baadaye huyu mtuhumiwa alitaka kumwingilia mwenzake kinyume na maumbile lakini marehemu alikataa.

“Ghafla kundi la wanaume lilitokea upande mwingine wa korongo ambao walimlazimisha marehemu akubali...wote walimkataha huyu marehemu na kuanza kumwingilia mmoja mmoja kinyume na maumbile hadi kusababisha kifo chake papo hapo,” alisema.

Aliongeza kuwa, wapita njia walikuta mwili wa mwanamke huyo ukiwa uchi nguo zake zikiwa pembeni akiwa ameonekana ambapo hadi sasa, jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi wa kina.


“Hadi sasa tunamshukia mtuhumiwa pekee ambaye alikutwa kwa mganga wa kienyeji akipewa dawa ya kumzuia asikamatwe na polisi, atafikishwa mahakamani wakati wowote,” alisema.

No comments:

Post a Comment