14 January 2013

Likokola mbunge aliyewakomboa Watanzania kupitia VICOBA


Na Gladness Mboma

BAADHI ya Watanzania nchini wameanza kunufaika na mpango wa .......(VICOBA) ulioanzishwa kwa kunufaika na maendeleo.

Uanzishwaji huo umewezesha kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kupambana na umaskini kwa kutumia vyanzo vya mapato katika maeneo yao chini ya mpango huo.

Toka kuanzishwa kwa mpango huo Watanzania wamekuwa wakipata elimu ya jinsi ya kujiunga na Vicoba, ili kujiongezea kipato chao kwa kutumia vyanzo vinavyowazunguka katika maeneo yao.

Uanzishwaji wa mpango huo kumewezesha wananchi kupata elimu ya jinsi ya kupambana na umaskini na kujiingizia kipato, ambapo wananchi wengi wameanza kunufaika nao kwa kuiona faida yake.

Mpango huo umetokana na Serikali ya Tanzania kupata ufadhili kutoka nchi tano kwa ajili ya kuiwezesha kutoa elimu kwa wananchi ya jinsi ya kupambana na umaskini kwa kutumia vyanzo vya mapato katika maeneo yao chini ya mpango wa Vicoba.

Mpango huu wa Vicoba umewanufaisha kwa kiasi kikubwa wananchi wa vijijini kutokana na wananchi wake hasa wanaoishi vijijini huonekana hutegemea kilimo na mifugo pekee licha ya kuwapo kwa fursa nyingi wanazoweza kuzitumia ili kuondokana na umaskini.

Jukumu lingine la mradi huo ni kupeleka vifaa vya kuhifadhia fedha katika kila kijiji pamoja na kuwahamasisha wananchi kujiunga kwenye vikundi vya watu 30 na kila mwanakikundi kununua hisa kuanzia sh.1,000 kwa mwezi na baada ya hapo kuanza kukopeshana.

Kutokana na mpango huo Watanzania wengi hususan wanawake ambao wanaonekana kuitikia kwa wingi kujiunga nao wamenufaika kwa kiasi kikubwa.

Rais wa Vicoba Tanzania Bi.Devota Likokola amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha Watanzania kujiunga na mpango huo ambapo amekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania.

Hakuna asiyemfahamu Bi.Likokola ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma alianza kazi hii ya uhamasishaji wananchi kujiunga na mpango huo kama utani,lakini amekuwa mmoja wa viongozi ambao amekuwa mstari wa mbele kupigania umaskini.

Bi.Likokola alianza kuhamasisha Watanzania kujiunga na mpango huo ambao kwa asilimia kubwa wengi walikubaliana na mpango huo ambao umekuwa ni faida kubwa kwao na umewaondolea umaskini hususan wanawake.

Wakati aliposhiriki chakula cha walemavu Diamond Jublee ambacho uandaliwa kila mwaka na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPP Bw. Regnald Mengi walizungumzia jinsi gani watakavyoweza kuwakwamua walemavu kuondokana na umaskini kwa wao kujiunga na Vicoba.

Nakumbuka Bi.Likokola alimhakikishia Bw.Mengi kuwa atakuwa mstari wa mbele kuakikisha kwamba anawaunganisha walemavu katika mpango huo ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kujiunga nao.

Kwa kuwa alipania kufanya hivyo hakika alifanisha hilo na walemavu wameitikia mpango huo na wamejiunga kwa wingi na Vicoba na kuchangia kwa wakati ambapo sasa wengi wao wameondokana na masuala ya kuomba omba kama ilivyokuwa zamani.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Bi. Lukokola amefanya kazi kubwa ya kuheshimika kwa serikali, kwani ni kiongozi mwanamke aliyeamua kujitolea kwa moyo mmoja kuhakikisha kwamba Watanzania wanaondokana na umaskini.

Maeneo mbalimbali mikoani sasa hivi kuna vikundi mbalimbali vya Vicoba, wanawake wananunua hisa, hali iliyosababisha sasa kuondokana na utegemezi waliokuwa nao mwanzo kwa waume zao.

Nakumbuka siku moja alikuja Maeneo ya Kimara Mavurunza kuja kufungua Vicoba vya wanawake, alishangazwa na jinsi wanawake walivyokuwa wamependeza, anastahili kupongezwa.

Unapokuwa unaamua kufanya kazi kwa moyo mmoja tena ule wa kuwatumikia Watanzania bila kinyongo utambue Mungu naye anakuwa upande wake, mimi namsifu Mbunge huyu kwa kujitoa.

Kazi ya uhamasishaji watu kujiunga na kikundi fulani na kutoa fedha zao jamani siyo mchezo inataka moyo, ninaimani kazi hii imepata mafanikio makubwa kutokana na ucheshi alionao mbunge huyu.

Wapo baadhi ya watu watakaoniuliza mbona ninasifu hivi, nimejionea kwa macho yangu jinsi alivyo mcheshi wakati anapokuwa akiwaeleza wananchi faida ya Vicoba, anakuwa karibu naye ana majivuno ni mnyenyekevu na ndio maana ameweza kupata mafanikio makubwa.

Tumejionea vitu vingi ambavyo wamepewa baadhi ya viongozi kuanzisha wameshindwa kuviendeleza na badala yake vimeishia hewani, hiyo yote inatokana na kutokuwa na uchungu na nchi yao.

Bi. Likokola anauchungu na nchi yake na ndiyo maana ameweza kusimamia kwa umakini wa hali ya juu hadi kufanikisha kwa kiasi kikubwa malengo yaliyotakiwa hivyo kuna kula sababu ya kumsifu kwa kazi yake kubwa aliyoifanya.

Ninampongeza hata Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Bw. Mengi amekuwa mstari wa mbele kusaidia vikundi mbalimbali katika mpango huu, kwani kwa kiasi kikubwa amefanikisha mpango huo.

Nakumbuka Bw.Mengi alilivalia kibwebwe suala hili la Watanzania kujiunga na Vicoba, mara nyingine alikuwa akiongozana na Bi. Likokola na kweli wameweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu kazi hiyo wameamua kuifanya kwa moyo mmoja kwa lengo la kukwambua Watanzania kuondokana na umaskini.

Hivyo basi viongozi hawa wanatakiwa kutiwa moyo na kuungwa mkono kwa juhudi zao kubwa wanazozifanya, tukumbuke kwamba ni Watanzania wengi ambao walikuwa hawana kazi za kufanya, lakini kwa sasa baadhi wanafanya baishara kwa kujiunga na Vicoba.

Wanawake wamekuwa sasa ndio msaada mkubwa katika familia zao kwa kujiunga na mpango huu,kuna kila sababu ya viongozi hawa kupongewa na kuungwa mkono kwa kazi kubwa wanayoifanya katika jamii.

Iwapo viongozi wote Tanzania wangekuwa na moyo wa kufanya kazi kwa moyo mmoja kama ilivyo kwa Bw. Mengi na Bi.Likokola, hakika Tanzania ingekuwa nchi nyingine isiyotajwa katika nchi mojawapo iliyokithiri kwa umaskini.

Nasema hivi kwa sababu Vicoba vimesaidia watu wengi kuweza kujiajiri na kuondokana na suala la kukaa vijiweni na wengine kutegemea waume zao, hii yote inatokana na utendaji kazi mzuri wa viongozi hawa.

Mimi binafsi nimefurahishwa na hali hiyo, baada ya kuona walemavu waliokuwa ni mzigo mkubwa kwa serikali kwa sasa kuanza kujitegemea kutokana na kupewa elimu na hivyo na wao kujiajiri baada ya kujiunga na mpango huo.

Kilichonifurahisha zaidi ni pale, Bi.Likokola alipokuwa akimweleza Bw. Mengi kuwa wameweza kuwakusanya ombaomba kutoka maeneo mbalimbali na kuwapa elimu jinsi gani ya kujiunga na Vicoba na wengi wao wameitikia mwito huo na wameondokana na suala lao la kutegemea kuombaomba.

No comments:

Post a Comment