14 January 2013

Umakini wa Zitto tumaini la Taifa (8)



Na Gladness Mboma

WAPENDWA wasomaji wa makala hii nina imani kila mmoja anaendelea kuifuatilia kwa makini na leo nitaendelea na sehemu ya nane inayohusiana na mahojiano kati ya wanachama wa Jamii Forum na Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Bw. Zitto Kabwe kuhusiana na mambo mbalimbali yanayohusiana na siasa
   

Siku ya kwanza tu nimeingia Bungeni sikulipenda. Hamu iliniisha. Lakini nikasema ngoja nibadili modus operandi ya Bunge. Nikaanza kutoa hoja kali kali Bungeni na hatimaye nikasimamishwa Bunge. Nafurahi kwamba Wabunge wengine walifuata kasi yangu.

Mnakumbuka kuna wabunge walikuwa wanasema ‘hatuwezi kumwachia Zitto Kabwe peke yake kazi ya kuibua ufisadi’. Sasa baada ya kuona nimefanikiwa nikasema basi term moja inatosha. Badaye nikapata ushawishi kuwa hapana, nenda Geita au Kahama au Kinondoni.

Nikafanya utafiti wangu nikaona mwenyewe kuwa niende Geita. Viongozi wa chama kutoka Geita wakaenda kuwaona wenzao Kigoma wakakataliwa. Wazee wakanikumbusha kuwa, makubaliano yetu yalikuwa mihula 2.

Ikabidi nitimize ahadi hiyo ya mihula 2. Haikuwa matakwa yangu. Mpaka sasa nime abandon PHD yangu maana sina muda na siasa zangu mimi huwa naacha kila kitu kinacho weza kuni divert, hivyo nakosa muda wa kusoma na kuandika.

SWALI:Tokana na kauli yako hivi karibuni kuhusu kwamba Uongozi wa nchi hautakiwi kuwa mikononi mwa watanzania waliozaliwa kabla ya uhuru; Je kulikuwa na ulazima kutamka haya?

Huoni kwamba iwapo utafanikiwa kuwa rais wa nchi yetu, urais wako unaweza kuja kutuletea generational conflicts (misuguano/migongano/mifarakano ya vizazi)?

JIBU:Mimi ninaamini kabisa kuwa Rais ajaye wa Tanzania ni lazima atokane na kizazi cha baada ya uhuru. Nchi inahitaji a fresh start. Misuguano ndio huleta maendeleo.

Hebu tazama nchi hii, Asilimia 70 ya Watanzania wapo chini ya umri wa miaka 29! Asilimia 65 ya wapiga kura wapo kati ya umri wa miaka 18 – 40. Hili ni Taifa la vijana.

Nusu ya Watanzania wapo chini ya umri wa miaka 17! Unaweza kusema hili ni Taifa la watoto. Hawa wazee wetu walipokuwa wanachukua nchi walikuwa vijana. Mwalimu alikuwa Waziri Mkuu akiwa na miaka 39, Mzee Kawawa alikuwa Waziri Mkuu akiwa na miaka 37.

Waziri Mkuu wakati huo ndio alikuwa Mkuu wa Serikali maana Mkuu wa nchi alikuwa Malkia wa Uingereza. Angalia mafanikio ya Mwalimu Nyerere na Kawawa kati ya mwaka 1961 na 1971 halafu pima na baada ya hapo mpaka wanastaafu.

Tusibwabwaje tu bila evidence. Ndio maana leo Marekani Rais wao ni kijana. Uingereza Waziri Mkuu wao kijana ingawa mataifa haya yana wazee wengi zaidi kuliko sisi.

Ninaweza kutamba kwamba mimi ni mmoja wa wanasiasa ambao ninaheshimu sana wazee. Uliza wazee waliopo na waliokuwapo Bungeni ni mwanasiasa gani kijana anatumia muda mwingi nao.

Mwulize mzee Sarungi, bahati mbaya mzee Makwetta amefariki. Mwulize dokta Salim, mwulize Mzee Warioba. Wao pia wananiambia, Zitto huu ni wakati wenu. Sisi tulifanya yetu.

Kuna watu lazima watafsiri chochote atakachosema Zitto. Hata hili ninaloandika hapa mtasikia, watasema tu. Kuna watu wanaumwa ugonjwa wa zittophobiasis ni lazima waseme.

Mtasikia tu wanasema hivi sasa. Sasa wanaotaka kutafsiri kauli yangu wana mambo yao, lakini ninaamini kabisa kuwa changamoto za sasa za Taifa zinahitaji Rais wa kizazi cha baada ya Uhuru. Wazee watatupa ushauri.

This country has to move very fast. We need an ambitous young man, visionery and focused to transform this country. Tunaweza kuwa na Spika mzee ili adhibiti kasi kama inakwenda sana, lakini sio CEO wa nchi. How Old was Lumumba? How old was Kagame? How old is Kabila?

Let us be serious guys. Mnataka tutambae? Wazee wameishi maisha yao. Wameishi yetu na sasa tunataka kuwakopesha maisha ya watoto wetu?

O: Zitto na "Ufisadi na Malimbikizi ya Mali" & "Pesa Uswisi"

SWALI:Unaposema kuwa ni jitihada zako mwenyewe za kupata hayo majina ya mafisadi wa Uswisi si inakuwa sawa na kuwa una maslahi yako binafsi kama vile kutaka kuyauza hayo majina kwa wale ambao wapo kwenye list?

Nadhani hivi ndivyo ungefanya wewe maana wakati mwingine watu hudhani vyao kwa wengine.

SWALI:Unachukuliaje mawazo/kauli ya baadhi kuwa kuwasilisha kwako hoja hiyo ya fedha za Uswizi bungeni bila kutaja majina ni moja ya njia ya kujisafisha katika uvumi/tetesi ya kuwepo katika list hiyo ya wenye fedha Uswizi?

JIBU:Kwangu mimi suala hili ni pana na majina ni sehemu tu ya suala hili. Nimeshasema mara kadhaa kwamba, nina akaunti mbili hapa nchini, CRDB na NMB. CRDB kwa ajili ya mshahara wangu na NMB kwa ajili ya fedha za kujikimu ninazolipwa na Bunge. Sio tu Uswisi, hapa Tanzania sina akaunti benki nyingine yeyote ukiachana na kuwa signatory kwenye akaunti za chama au za kifamilia.

Sina biashara yeyote hapa nchini au nje ya nchi. Naishi kwa mshahara na siwezi kuupeleka mshahara Uswisi. Waliosema mimi nina fedha huko Uswisi walikuwa na lengo la kufifiza hoja yangu kwa malengo yao.

Ni watu waliotumwa na usalama wa Taifa au na wenye fedha ili niogope. Watu wa aina hii ni wapuuzi, wapumbavu na hatari sana kwenye vita dhidi ya ufisadi. Tena watu hawa mnawajua na mnawachekea. Hawa watu ni vibaraka wa watu fulani.

Tena nasikia wametengeneza na orodha yao ya wenye fedha nje. Hawa ndio wagonjwa wa zittophobiasis. Nasikia wengine walisema kuwa hii hoja akiachiwa Zitto itampa umaarufu. Wapuuzi wanawaza umaarufu tu badala ya kuwaza nchi yetu.

Suala la utoroshwaji wa fedha kwenda nje ni kubwa sana. Tanzania imepoteza dola bilioni 11 toka mwaka 1970 mpaka sasa (ukiongeza na riba kwenye fedha hizo). Halafu kuna wapuuzi fulani wanaleta uzezeta kwenye masuala ya msingi ya nchi.

Wanajijua ninaowasema hapa. Waache ujinga. Kama humpendi Zitto basi penda afanyacho kwa maslahi ya nchi yetu.

SWALI:Kuna ukweli wowote kuwa taarifa ile ya USWISI kuiwekea masharti Tanzania, ilitoka ndani ya serikali ya USWISI au ni mkakati wa mafisadi hawa kuzima jaribio la kurejesha pesa hizo?

JIBU:Nimetoa kauli jana kuhusu suala hili. Nimesema Watanzania tusiwe mazezeta. Kauli hizi ndio ambazo hata Marekani waliambiwa. Hata Ujerumani waliambiwa.

Sisi kuzishabikia badala ya kufanya uchunguzi wetu kwa njia zetu ni dalili za kutaka kuua hoja hii. Hoja hii haitakufa. Tutaisimamia mpaka mwisho.

SWALI:Je, kuna nafasi ya nchi yetu kufanikiwa kuyarejesha mabilioni hayo ambayo ni kodi ya wanachi?

JIBU:Tunaweza kurejesha. Kuna Azimio la Bunge na nitahakikisha Azimio la Bunge linatekelezwa. Senegal wanafanikiwa sana. Kenya walifanikiwa kwa kutumia wachunguzi binafsi.

Kama Serikali ya CCM itashindwa kufuatilia suala hili, Serikali ya CHADEMA itafanya hivyo. Hawana pa kujificha katika dunia ya sasa.

SWALI: Ikumbukwe kuwa, tangu nchi hii itumbukie katika ufisadi mkubwa, chombo chetu TISS kipo kama hakipo, na kama kipo basi ni kwa msaada wa mafisadi tu, Katika mtazamoo na tafsiri ya ripoti yako, taasisi ya Usalama wa Taifa (TISS) Unaiweka katika mizani ipi au haihusiki katika hili?
 *********
JIBU:Idara ya Usalama wa Taifa ni lazima isaidie nchi kwenye masuala kama haya, vinginevyo hawapaswi kuwepo. Sheria ya TISS ya mwaka 1996 inawazuia kuchukua hatua fulani fulani.

Tutarekebisha sheria hiyo. CCM wasiporekebisha sisi CHADEMA tutapata ridhaa ya wananchi kuiandika upya sheria ya Usalama wa Taifa. Tunataka usalama wa Taifa na sio usalama wa viongozi au vyama vya siasa.

SWALI:Kwanini umependekeza kuundwa kwa tume, na kuendelea kumaliza pesa za watanzania wakati kimantiki ripoti yako ilikuwa ni ya kuiwasilisha vyombo vya dola tu, na ikiwa hawajaridhika, TAKUKURU kwa utaratibu wao wa ndani waendeshe uchunguzi na kuchukua hatua?

JIBU:Uzuri wa Kamati Teule ya Bunge ni kwamba kila kitu huwa wazi kwenye hansards za Bunge na hivyo ni rahisi kufichua uchakachuaji. Pia ngoja niwamegee siasa za Bunge kidogo. Bungeni unapokuwa na hoja unaingia na hitaji kubwa sana wakati unajua fall back ni nini.

Tulijua kwa hatua ya sasa hawatakubali kuundwa kwa kamati teule, tulitaka hoja ipite ili kujenga msingi wa kupanua uchunguzi siku za usoni.

Tukafanikiwa. Tulitumia approach hiyo hiyo kwenye hoja ya ndugu Halima Mdee. Ni mikakati tu. Sisi tumekuwa ni Bunge la kwanza katika eneo la SADC kutoka na Azimio kuhusu 'illicit money flows'. Sasa tunapaswa kuhakikisha Azimio linakuwa enforced na kisha a public inquiry....

SWALI:Huku ukijua serikali haina nia ya kuwataja walioficha fedha mabenki ya nje huku wewe ukiwa na majina; unayashikilia hadi sasa ili nini na kwa faida ya nani?

Kwa faida ya uchunguzi. Lazima Serikali ijenge uwezo wake wa kuchunguza na kuweka mambo sawa baada ya uchunguzi. Sasa ikiwa mimi kama mbunge nitatoa jina la walio torosha pesa kwa sasa, nani atatoa majina hapo kesho?

SWALI:Ni ukweli kuwa wewe ni mshauri wa uchumi wa Ujerumani. Kama ni kweli, je ni kitu gani kilichokutambulisha hadi kufikia kupewa hiyo nafasi?

JIBU:Nilikuwa kwenye jopo la Rais Kohler kuhusu Afrika. Nilimaliza kazi hiyo mwaka 2009. Niliteuliwa tu na Rais Kohler wa Ujerumani

  

No comments:

Post a Comment