18 January 2013

Lema kutoshirika ziara za Kikwete


Na Martha Fataely, Moshi

SAKATA la kukataliwa kwa Meya wa Jiji la Arusha, Bw. Gaudence Lyimo, sasa limekuchukua sura mpya baada ya Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema (CHADEMA), kutangaza nia yake ya kutoshiriki ziara za Rais Jakaya Kikwete, mkoani humo kama
Bw. Lyimo atakuwepo.


Bw. Lema aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Railway, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ambapo chama hicho kilifungua matawi
mapya zaidi ya 20 jijini humo.

Alisema msimamo wake na chama chake ni kwamba, Bw. Lyimo alichaguliwa katika nafasi hiyo kwa njia isiyo halali. “Sitashiriki ziara ya Rais Kikwete jimboni kwangu kama Meya huyu atakuwepo, ikitokea nimeshiriki tutavunjiana heshima,” alisema.

Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa Njoro, Kwa Mtei na Majengo,
Bw. Ali Athumani, Bw. Habibu Miraji na Bi. Magreth Shirima walimshangaa Bw. Lema na kudai anatafuta umaarufu kwani kutoshiriki ziara hizo ni kukwamisha maendeleo ya wananchi.

Katika hatua nyingine, Bw. Lema alimtaka Meya wa Manispaa ya Moshi, Bw. Japhary Michael, kushinikiza mabadiliko ya msimamo wa Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Bw. Bernadette Kinabo ambaye anadaiwa kuzuia juhudi za CHADEMA kutekeleza ilani yake.

Kwa upande wake, Bw. Michael alidai Bi. Kinabo amekuwa akikwamisha juhudi za chama kuharakisha maendeleo ya
wananchi mbali ya chama hicho kuandaa mazingira mazuri
ya kibiashara kwa wafanyabiashara ndogondogo wa Moshi
lakini amekuwa akiwafukuza na kuporwa mali zao.

Wakati huo huo, Mbunge wa Arumeru Mashariki, mkoani Arusha Bw. Joshua Nassari (CHADEMA), amesema kama chama hicho kitashika dola katika Uchaguzi Mkuu 2015, na kuteuliwa katika
nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, atawakamata
baadhi ya viongozi wa Serikali wanaodaiwa kujihusisha na
vitendo vya ufisadi ili waweze kurejesha fedha za wananchi.

Bw. Nassari aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Njoro, Manispaa ya Moshi, mkoani humo na kudai kuwa, wapo baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wanaofuja fedha za Serikali.

Alimuomba Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa, ampe Wizara hiyo kama chama hicho kitashika dola mwaka 2015
ili aweze kuonesha mfano wa utendaji na kuwaondoa baadhi ya viongozi ambao si waadilifu.

“Kila nikipita mitaani, nawaona wafungwa  wengi watarajiwa, wapo watu ambao haijulikani wanapata wapi fedha lakini ni matajiri wa kutisha, nipe nafasi angalau ya wiki moja niwashughulikie.

“Naomba Katibu wangu usinihoji suala la mimi kuona, hivi sasa mawazo yangu nimeyaelekeza kwa Watanzania jinsi ninavyoweza kuwakomboa katika lindi la umaskini walionao,” alisema.

Alisema umefika wakati wa viongozi kutafakari maendeleo ya Taifa kwani wananchi wameendelea kuwa maskini kwa zaidi ya miaka 50 licha ya Tanzania kuongoza kwa uzalishaji madini ya Tanzanite.

Aliongeza kuwa, mbali ya madii pia kuna dhahabu, gesi, makaa ya mawe, mbuga za  wanyama na Mlima Kilimanjaro ambavyo vyote vinaweza kuondoa umaskini uliopo kwa Watanzania kama rasilimali hizo zitasimamiwa vizuri kwa masilahi ya Taifa.

9 comments:

 1. umekuwa nje ya bunge muda mrefu, maendeleo ya jiji la arusha yako chini, bado unagoma kutoshiriki shughuli zinazoleta maendeleo. unamkomoa nani? ukweli ni kwamba mheshimiwa ndiye mwenye nyundo kwa wakati huu.
  Nchi za kiaafrika tutafute dawa ya kupata viongozi bora. CCM, CHADEMA, CUF wote ni wazee wa madini.

  ReplyDelete
 2. Amekuwa nje ya bunge muda mrefu, maendeleo ya jiji la arusha yako chini!!!!
  KWELI AMEKUA NJE YA BUNGE MUDA MREFU LKN AKIWA NJE UNAJUA KAZI ZILIZOKUA ZIKIENDELEA,JE UNAUHAKIKA GANI MAENDELEO YA ARUSHA YAKO CHINI,UNATUMIA KIPIMO KIPI?

  ReplyDelete
  Replies
  1. we nawe uko lala, huoni moshi ni safikuliko arusha? huitaji vigezo vya kisayansi kujua kuwa arusha bado tuko nyuma, kwakopa pale ni jiji lakini wenzako wanaojua maana ya majiji huwezi kusema arusha au mbeya ni majiji, bado ngazi ya halimashauri. Angalia barabara, uchafu, majengo shaghla baghala, huduma za maji safi, usafiri banabana vipanya, kaeni sita siti ya watu wannne, mengine utajaza,,,,

   Delete
 3. Ninaposema chadema ni chama cha wasanii wa wafanyabiashara sikosei.Kwa hili analolisema Lema ni upuuzi mtupu na watu wenye akili wameelewa sasa kuwa chadema sio chama cha kutetea wala kuleta maendeleo kwa wananchi bali ni chama cha porojo, uongo uongo,wiziwizi na udakuudaku.

  Ninawashauri wakazi wa Arusha wafanye maamuzi magumu katika uchaguzi ujao kwa kukikataa chadema na kuangalia chama kingine kinachoweza kufanya kazi za wananchi.

  Bonafsi nashauri zamu ijayo iwe ya CUF sasa maana CCM tumeiona miaka nenda hakuna jipya, Chadema nayo miaka mitano imepotea bure nguvu za wapiga kura zinachezewa na watu watatu tu, sasa tuseme chadema BASI KARIBU CUF.

  ReplyDelete
  Replies
  1. ARUSHA,HAKUNA CHA CUF AU CCM,NI CHADEMA MBELE KWA MBELE,KAMA HUTAKI CHAGUA CUF YAKO TUONE KAMA UTASHINDA.KWANI MAENDELEO YANALETWA NA KUHUDHURIA MIKUTANO YA CCM NA MWENYEKITI WAO.HATA BILA KUWA KWENYE MSAFARA WA RAIS MAENDELEO YATAPATIKANA.MMEZOEA SANA OMBA OMBA,HATA PESA ATAKAZOTUMIA KWENYE MAENDELEO NI KODI YA WANANCHI,NA SIYO YA KIKWETE.

   Delete
 4. Bila kujishirikisha hutaweza kujenga jiji la Arusha, dawa siyo kususia ila ni kushiriki na kupanga mipango ya kurekebisha makosa na siyo kukimbia makosa. Kaa na meya ili umjue na kumrekebisha wakati wa uchaguzi.

  ReplyDelete
 5. rema yuko sahihi, nani asiyejua kama lyimo ni meya feki, ni vizuri zaidi kusimamia UKWELI, na siyo kukubali uongo kwa maslahi ya watu wachache, mtu anayetakiwa kujitathimini ni meya lyimo je yuko pale kikatiba au ni kwa masilahi yake na chama chake, LEMA YUKO SAHIHI, ENDELEA KUSHIKILIA UKWELI KULIKO UONGO USIO NA MAANA.

  ReplyDelete
 6. HAINGII AKILINI IKO KAULI WATU WOTE WAKIFUMBA MIDOMO WAKIACHA KUONYESHA MATENDO YAO SI RAHISI KUMUELEWA TAAHIRA WALA KICHAA TUNASHUKURU MUNGU KWA KARAMA HIYO TUMEWEZA KUMFAHAMU MBUNGE NI MTU WA AINA GANI MBONA MWENYEKITI WAKE ALIMKARIBISHA RAIA KULE HAI TUACHE UZEZETA MBONA UNAKEMEWA SANA HAPO ARUSHA PAMOJA USUKULE

  ReplyDelete
  Replies
  1. KWELI MBOWE ALIMKARIBISHA RAIS KIKWETE KULE HAI WAWE WANAHUDHURIA LIVE MAHUBIRI YA RADIO SAFINA NA WALA SIO KUSIKILIZA KWENYE RADIO KAMA WATU WA MASAFA BILA HIVYO USUKULE NA UZEZETA UTAZIDI KUWANDAMA IKO KAULI NABII HATABULIKI KWAO

   Delete