28 January 2013

Kila shule iwe na mabweni-TGNP


Na Mariam Mziwanda

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeeleza umuhimu wa kuwa na sera itakayowezesha kila shule nchini kuwa na mabweni ya wasichana ili kuwaandaa wanawake katika kutekeleza mpango wa maendeleo wa dunia.

Hayo yalielezwa jana jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa TGNP ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilianio, Bi. Lilian Lyundi wakati wa maadhimisho ya siku ya msichana wa shule ya sekondari Royola.

Bi. Lyundi alisema kuwa kuthamini mtoto wa kike ni vyema kuwendane na sera itakayoweka mikakati ya wasichana kupewa mazingira mazuri ya kupata elimu ili kuwawezesha vijana wa kike kutengeneza dunia ya maendeleo.

"Wasichana ni viongozi na wamezaliwa kuwa viongozi kuanzia wa majumbani na kwingine, hivyo uwepo wa sera ya mazingira bora ya kupata elimu sanjari na kuwepo kwa mabweni katika kila shule kutapelekea kumwezesha mtoto wa kike katika kutengeneza
nchi na dunia kwa  maendeleo,"alisema

Alieleza umuhimu wa wanawake kujengewa jinsi ya kujipanga katika mikakati ya baadae ili waweze kuongoza jamii ni mkubwa ikiwa sambamba na kupewa elimu ya mara kwa mara jinsi ya kuondokana na vikwazo vya ugumu wa maisha.No comments:

Post a Comment