21 January 2013

Katibu wa CHADEMA ahamia NCCR



Na Darlin Said

ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Mbeya, Bw. Eddo Makata, ametangaza rasmi kujiunga na chama
cha NCCR-Mageuzi.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bw. Makata alisema, ameamua kuhamia chama chake cha zamani
baada ya kukerwa, kuchoshwa na ufisadi pamoja na ukiukwaji
wa katiba unaofanywa na viongozi wa CHADEMA.

Alisema ndani ya CHADEMA, kiongozi anapotofautiana na
wenzake kwenye mambo ya msingi, anaonekana msaliti wakati mwingine kuitwa majina ya kudhalilishana.

Aliongeza kuwa, sababu nyingine zilizomkimbiza katika chama hicho ni pamoja na viongozi kupenda sera za CCM za zidumu fikra za mwenyekiti hata kama ni mbovu.

Alitoa mfano na kudai kuwa, katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, wanachama wa CHADEMA walipohoji sababu za Bi. Josephine Mshumbushi (mchumba wa Dkt. Wilbroad Slaa), kutengewa fedha kwa ajili ya kufanya ziara za kumpigia kampeni Katibu Mkuu,  baadhi yao walionekana wabaya.

“Kitendo cha mchumba wa Dkt. Slaa kutengewa bajeti, kwenda mikoani na kupokelewa kama mke wa Rais kimenisikitisha sana,
jambo hili halijapata baraka za vikao...huu ni ubadhirifu mkubwa
wa fedha na utoaji posho kinyemela.

“Mwanachama anapohoji ubadhirifu huu anaambiwa pandikizi wa CCM bila kujali haya ni matumizi mabaya ya fedha,” alisema.

Aliongeza kuwa, mfadhili wa chama hicho Bw. Mustapha Sabodo, alitoa mamilioni ya fedha kukisaidia chama ili kijenge chuo lakini hazikutumika kwa kusudio hilo na unapohoji, unaambiwa
zimetumika katika operesheni za M4C.

Alisema chama hicho kina matumizi mabaya ya ruzuku na upendeleo wa kuzigawa kwenye majimbo akitolea mfano wa
Jimbo la Ubungo kuwa linapewa sh. 800,000 kila mwezi wakati majimbo mengine kama Kyela, mkoani Mbeya yanapewa sh. 100,000.

Bw. Makata alisema jimbo hilo linapewa fedha nyingi kwa madai ya kuwapa upaarufu hivyo kutokana na hali hiyo ni wazi kuwa chama hicho hakina dhamira nzuri ya kuleta mabadiliko kama kinavyodai.

“Uamuzi wangu kuhamia NCCR-Mageuzi ni mwanzo tu, wengine wengi watanifuata, siasa za maji tak hazifai kwenye upinzani, siasa uchwara zilizokuwa CCM...hivi sasa zimeingia CHADEMA, watu wanafukuzana hovyo na hakuna kuheshimiana,” alisema.

Kwa upande wake, Katibu Mwenezi na Mahusiano ya Umma wa NCCR-Mageuzi, Bw. Moses Machali, alisema vyama vya siasa lazima vijitathmini jinsi ya kuwahudumia wananchi.


3 comments:

  1. uchaguzi mkuu ulifanyika mwaka 2010; leo ni takiribani miaka miwili, eddo alishindwa nini kuueleza umma kupitia vyombo vya habari kama kuna matumizi mabovu ya mke wa silaa wakati wa kampeni, pia alitakiwa kujiodoa katika chama kwa tuhuma hiyo tungejua kweli anasaka mabadiliko, kwa sasa ni uchu wa madaraka unamsumbua baada ya kuona changamoto ya vijana wenye uwezo ktk chama.

    ReplyDelete
  2. UFISADI USIPAMBWE HAUNA RANGI HAUNA SURA KUPATA CV YA KUSHIKA DOLA NI KUVUTIA WATANZANIA KWA REKODI ISIYO NA HARUFU YA UFISADI

    ReplyDelete
  3. Kijana hakuna atakaye kufuata umeenda pekeyako sisi tunasonga mbele kusaka mabadiliko ktk nchi hii ulikuwa wapi kuyasema hayo yote kama ni kutoka 2010 ulisubiri utimuliwe ndio uyasema wasalimie huko ccm C.

    ReplyDelete