21 January 2013

DC ataka mazungumzo kuhusu gesi


Na Godwin Msalichuma, Mtwara

MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Wilman Ndile, amesema upo umuhimu wa kuzungumza na wananchi wa kada mbalimbali  mkoani humo kuhusu suala la gesi ili kuleta utulivu na amani katika halmashauri zote za Mkoa huo.


Ndile aliyasema hayo jana kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara ambacho kimefanyika hivi karibuni.

“Mimi naona ipo haja ya kuleta watalaam kutoka Wizara ya Nishati na Madini ili watu wapate majibu yanayowasumbua wananchi kuanzia ngazi ya chini kabisa,” alisema Ndile.

Alisema wananchi hawawezi kuandamana kama watapata majibu ya uhakika kuhusu masali yao ili waendelee na shughuli zao hasa za kilimo mashambani.

Aliyashukuru mashirika na watu binafsi mkoani humo kwa michango waliyoitoa baada ya maafa ya mvua zilizosababisha uharibifu mkubwa.

“Zaidi ya kaya 2,000 ziliathiriwa na mafuriko, katika historia ya Mkoa huu, mvua hizi hazijawahi kunyesha zaidi ya miaka 24 iliyopita, ilinyesha kiasi cha milimeta 104.18 kwa mujibu wa Kituo cha Naliendele mkoani hapa,” alisema.



No comments:

Post a Comment