28 January 2013

Bulembo ataka walimu kusimamia michezo


Na Andrew Ignas

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Abdallah Bulembo amewata walimu kuhakikisha wanasimamia sera ya michezo shuleni, ili kujenga Taifa lenye kuthamini michezo.


Akizungumza Dar es Salaam juzi mara baada ya kukabidhi mipira na nyenzo ya huduma ya kwanza, ambavyo vimeghalimu zaidi ya sh. 500,0000 kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Vituka, Mwenyekiti huyo alisema ili kupata vijana wenye uelewa mzuri na wa haraka, lazima wakuzwe na kulelewa katika michezo.

"Asilimia kubwa ya watoto wanaongoza darasani ni wale, ambao wanashiriki  michezo hii sera ya michezo shuleni ni kitu ambcho, kinatakiwa kupewa uzito wa aina yake," alisema Bulembo.

Alisema michezo ikipewa kipaumbele  itasaidia kuitangaza nchi kimataifa, pamoja na kutoa ajira kwa vijana badala ya kuongezeka wimbi la vijana wasio na kazi.

"Kuna vijana wengi, ambao wamepata ajira kupitia michezo na tangu wakiwa shuleni ambao majina yao bado yanajulikana ndani na nje ya nchi, hivyo Taifa linatambulika zaidi," alisema Bulembo.

No comments:

Post a Comment