16 January 2013
Bilal: Vifo vya uzazi nchini vimepungua
Na Queen Lema, Arusha
IDADI ya vifo vitokanavyo na uzazi nchini, vimepungua kwa asilimia 50 ukilinganisha na mwaka 2009 ambapo takwimu zinaonesha wajawazito 500 walipoteza maisha ambapo
mwaka 2010, vifo hivyo vilipungua na kufikia 250.
Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal aliyasema hayo
jana wakati akifungua mkutano wa Afya ya Mama, jijini Arusha
na kuongeza kuwa, lengo ni kupunguza vifo hivyo na kufikia
193 ifikapo mwaka 2015.
Alisema Serikali itajitahidi kuhakikisha lengo hilo linafikiwa ili kuhakikisha kwa kuzuia matatizo mbalimbali yanayochangia vifo vya wanawake wajwazito wakati wa kujifungua.
“Kupitia mkutano huo Tanzania itapiga hatua ya kupunguza vifo hivi kupitia utaalamu wa mataifa mengi yaliyoshiriki ili kuokoa maisha ya wanawake nchini,” alisema Dkt. Bilal.
Aliongeza kuwa, baadhi ya nchi zinashiriki mkutano huo tayari zimepiga hatua kubwa ya kupunguza vifo hivyo hivyo kupitia
nchi hizo ni wazi Tanzania itafanikiwa katika hilo.
Dkt. Bilal alisema takwimu zinaonesha kuwa, nchi nyingi za Afrika ambazo zinaendelea, zina idadi kubwa ya vifo vya uzazi ambapo kwa sasa vinafikia asilimia 99.
“Tanzania ipo tayari kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali ili kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na kuhakikisha wahapotezi maisha kutokana na uzazi au magonjwa ambayo
yanaweza kuzuilika,” alisema.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya na Ustawi nwa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi, alisema Wazira yake kwa kushirikiana na Serikali Kuu imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kila mwanamke anapata lishe kabla ya kubeba ujauzito ili aweze kupata nguvu za kujifungua na kuwa na afya bora.
Alisema changamoto inayosababisha vifo vitokanavyo na uzazi ni pamoja na usafiri ambapo wajawazito wengi hujifungulia njiani kutokana na umbali wanapokwenda katika vutuo vya afya.
“Kwa sasa Serikali itatoa vifaa vya kujifungulia bure ili wajawazito wote waweze kujifungua salama kwani wengi wao bado hujifungulia nyumbani wakiogopa gharama za kujifungua katika vituo vya afya,” alisema Dkt. Mwinyi.
Mkurugenzi wa asasi ya MDH, Dkt. Chalamila Guerino, alisema mkutano huo utatoka na maazimio ya kupunguza vifo hivyo na kuboresha huduma ya afya ili Tanzania iweze kufikia malengo
ya milennia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
A cry for our beloved professionalism, hivi mhariri mkuu na mhariri mtendaji na wahariri wa gazeti la majira mna ajenda gadi na CHADEMA?
ReplyDeletenI MUDA MREFU SANA MNAANDIKA STORY ZAO KWA KUZIPA KIPAUMBELE WAKATI KUNA VITU VINGI SANA VYA KUANDIKA? Barabara kibao zinajengwa muda mrefu hamtuandikii ni kwanini zinachelewa, Shule zimefunguliwa na wengine hawaanza kwa kukosa waalimu hamweki,
Kuna story nzuri za mikoani mnaweka ndani wakati zinawza kusaidia jamii husika kama, shule yakosa vyooo, mliiweka kurasa za ndani ila mnaona kuwa story za CHADEMA zinauza.
Acheni ujinga, unafiki na majungu, hiyo kampuni ina wenyewe mmeikuta na mtaondoka muiache,
TUmechoshwa na story za CHADEMA, kuwa front page. Huo si uandishi. Basi mjitahidi kubalance ili tupate ukweli maana mnatauchanganya. Kwani mnalipwa bei gani???????????????????????
JISAHIHISHENI, ma tuelezeni mapema kama ni gazeti la CCM. Gazeti huru ndio kila siku muandike CHADEMA?