Na Zubeda Mazunde
WIZARA ya kilimo kwakushirikiana na wadau wa kilimo wameandaa mkakati wa kuboresha zao la mpunga katika mabonde ya Kilombero mkoani Morogoro na Rufiji.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi,Mratibu wa mpango wa kukuza kilimo kanda ya kusini Bi. Marry Shatto alisema mkakati huo una lengo la kuboresha sekta ya kilimo katika zao la mpunga.
Alisema kuwa lengo kuu la kuwakutanisha wadau hao ni kuhakikisha wanaboresha uzalishaji wa mpunga kwa kutumia tekinolojia za kisasa ikiwa ni pamoja na uzalishaji mzuri kwa wakulima wadogowadogo nchini.
Bi. Shatto alisema kuna fulsa ya kuboresha zao la mpunga sababu sasa ndio zao linalopendwa na watu wengi, hata hivyo mpaka sasa wamefanikiwa kuzalisha zao la mpunga katika mabonde ya Kilombero na Rufiji Tani laki tano (5).
"Pia kuna fursa kubwa sana ya kuboresha ukoboaji wa mpunga ili kuwaridhisha wateja wetu, kwani kuna ukoboji wa mpunga unaosababisha mpunga kukatikakati kitendo ambacho si kizuri kwa masoko yetu.
"Tumeona wenyewe mchele unaokobolewa vizuri na ukiwa umenyooka unauzika masokoni kuliko ule unaokobolewa na kutoka vipande vipande, hivyo basi ipo haja kubwa ya kuboresha ukoboaji wa zao la mpunga nchini" alisema
Bi. Shatto alieleza changamoto zinazowakabili wakulima hususani wakulima wadogo wadogo kuwa ni kutokupata elimu ya kutosha kuhusu uzalishaji wa mazao pamoja na kutokuwa na mitaji ya kutosha kukidhi biashara zao.
Alieleza kuwa, kutokana na wakulima wengi kutokuwa na mitaji ya kutosha tumeamua kuanzisha mfuko utakao wasaidia wakulima wakubwa na wakulima wadogo wadogo nchini.
Naye Mkurugenzi msaidizi mtafiti wa mazao wizara ya kilimo mazao na ushirika Bw.Hussein Mansoor alisema licha ya kuboresha zao la mpunga, tunaangalia ni jinsi gani tutaweza kuongeza uzalishaji katika mfumo wa kutumia mbengu bora na sehemu inayostaili kupandwa zao hilo.
"Hali halisi ya zao la mpunga sio mbaya sana, ila tunatakiwa kuboresha zaidi sekta hii kwasababu ndio zao lenye soko hapa nchini" alisema.
No comments:
Post a Comment