05 December 2012

Nape achekelea ukweli wa Slaa *Ampongeza kwa kukiri kumiliki kadi ya CCM *Amtaka awaeleze wananchi ameilipia hadi lini


Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye, amempongeza Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kukiri kumiliki kadi ya chama chao hadi sasa.


Alisema Dkt. Slaa ameanza kujifunza kusema ukweli baada ya kutambua uongo haulipi kwani kitendo cha kukiri kumiliki kadi
ya CCM ni cha kiungwana hivyo anastahili pongezi.

Bw. Nnauye aliyasema hayo Dar es Salaam jana baada ya Dkt. Slaa kujibu tuhuma zake kuwa, wapo baadhi ya vigogo wa CHADEMA ambao wanamiliki kadi za CCM na wanazilipia hadi sasa.

“Dkt. Slaa amekiri katika vyombo vya habari kuwa anamiliki kadi ya CCM hadi sasa akidai anaitunza kama kumbukumbu muhimu hivyo ni vyema akawaeleza Watanzania kadi yake ameilipia hadi
lini na aache kuwadanganya wenzake warudishe kadi za chama tawala wakati yeye ameendelea kuwa nayo,” alisema.

Bw. Nnauye amekiri kumheshimu sana Dkt. Slaa kama babu yake na alishtuka sana kusikia Katibu Mkuu huyo anawatuhumu baadhi ya viongozi wa CHADEMA na kudai ni mamluki wa CCM wakati yeye ni namba moja kwani anaowatuhumu hawana kadi za chama hicho.

“Nilimsikia Dkt. Slaa akiwatuhumu baadhi ya viongozi ndani ya chama chao kuwa ni mamluki wa CCM, hili linawasaidiaje Watanzania maskini.

“Kitendo hiki kimethibitisha upeo mdogo alionao katika kufikiri, huyu ni kiongozi mkubwa ambaye namuheshimu lakini anapaswa kujua yeye anaomba kuwa kiongozi hivyo lazima wananchi tumjue tabia zake,” alisema Bw. Nnauye na kuongeza;

“Viongozi wa aina yake ni janga kwa Taifa letu, usipokuwa mwaminifu kwa kidogo, huwezi kuwa mwaminifu kwa kikubwa,” alisema.


19 comments:

  1. duuuuuh sasa kwa nini anawaambia watu warudishe kadi wakati yeye anamiliki? c kiongozi wa kweli

    ReplyDelete
  2. Hapa ndio maana Nape anaitwa VUVUZELA. Sasa ukibaki na kadi ya CCM halafu ukawa na maono kama ya Dr Slaa kuna tatizo gani?

    Ukibaki na kadi ya CCM, tena iko uptodate halafu ukasema si sahihi mbunge kulipwa seating allowance( Posho ya Vikao) kwa kazi ambayo ni jukumu lako kuna tatizo gani? Tatizo si kuvaa shati ya KIJANI au Combati ya kaki, Tatizo ni kuwa mnafiki kwa kuishi kifisadi huku ukiimba ujamaa na maneno matamu ya kumuenzi Mwl Nyerere.

    ReplyDelete
  3. Tatizo la Nape ni KUKOSA ADABU. Haya ndio matatizo ya watoto wasio na BABA tunamshauri nape akatafute BABA YAKE MZAZI kwani inajulikana kuwa MZEE NNAUYE sio baba yake. NAPE TUNAKUSHAURI UKATAFUTE BABA YAKO ILI UJUE KUHESHIMU WAKUBWA

    ReplyDelete
  4. Hivi kweli watanzania wakiulizwa nani ana upeo mdogo kati ya Nape na Dr Slaa watajibu nini? Haihitaji kuwa na degree kujua kuwa nape anaupeo mdogo hata mwanangu anayesoma chekechea atakueleza. Punguza mdomo nape, mdomo uliponza kichwa. Unatia kichefuchefu! We are tired of you!

    ReplyDelete
  5. Kwani Nape kwa hilo atafaulu kuwashawishi watanzania waache kukisema Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo vya rushwa na ufisadi.Kwa sasa vita ya CCM kukomesha rushwa na ufisadi imewashinda,kilichobaki wameamua kutangaza vita na wale wanaopiga vita rushwa na ufisadi.

    ReplyDelete
  6. nape na ccm yake utafikiri walizaliwa na mama mmoja, maana badala ya kuzungumzia issues wana attack mtu.ndio maana badala ya kutatua matatizo ya watanzania wanaanda njia kupata posho kwa kuanzisha kutembea nchi nzima.
    nape acha kuwa kama unapulizwa,maana vuvu zela ndio linapulizwa

    ReplyDelete
  7. Jamani Ukweli NAPE si mpendi ila nae ndugu yetu kajichanganya kweli, kuna haja gani kuitunza kadi ya Chama ambacho hukipendi na kuku unapanda jukwaani kila kukicha kuwaambia wengine warudishe kadi wajiunge na Chadema? Babu rudisha hiyo kadi haina maana kwako japo utakuwa umechelewa kwani tayari umekaliwa kooni japo uvuvuzela wa Nape ndio unaokusaidia kwani watu wamechoka na CCCCM

    ReplyDelete
  8. MUNGU HAMFICHI MNAFIKI NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO VIONGOZI WANAFIKI HAWAFAI KUONGOZA NCHI WALA TAASISI YOYOTE

    ReplyDelete
  9. WOTE HAKUNA KITU HAPO

    ReplyDelete
  10. CCM MMECHOKA 2015 MTATOKA TU NAPE CHUNGA MDOMO UNAPOTEZA POPULARITY ATTACK IDEAS AND NOY PHYSICAL APPEARANCE MBONA WAPO MANACCM WALITAKA KUJIUNGA CHADEMA NA CCJ NA WAPO SERIKALINI SASA BABU YUPO JUU

    ReplyDelete
  11. nape yupo sahihi sana hapa, kwa hili eeh yupo sahihi. tuache kutetea tu ili mradi kimefanywa na kionongozi tunayempenda..labda kabla ya kumhukumu aseme amelipia mpaka lini. hapo tutaangalia ni lini huyu amejiunga na kutoa maamuzi sahihi

    ReplyDelete
  12. Kwani kuwa na kadi ndio nini? Kadi ni kipande cha karatasi tu, na mtu anaweza kukiweka kama souvenir wakati anakichukia chama hicho. Hiyo kadi anawaze kuisokotea sonyo akipenda. Si lazima airudishe. Nape aongee mambo yenye tija kwa taifa hili na sio kuharisha maneno.. pruuuu pruuuuu pruuuu!

    ReplyDelete
  13. waungwana,ni kitendo,kwa mauno yangu hizi ni propaganda za siasa ,hakuna cha nape wala slaa!wote chungu kimoja,chadema kuchukua nchi hii ni sawa na kusema sasa nchi hii itawaliwe na watu wenye ufinyu wa fikara,kinachotakiwa ni ccm tu kujiweka sawa,watu kufanya kazi kwa bdii,chadema ni janga la taifa,hamuoni hilo ndugu zangu.

    ReplyDelete
  14. MIMI NAOMBA NITOKE NJE KIDOGO YA MADA,NIMZUNGUZIE LEMA MBUGE MTIMULIWA WA ARUSHA,JAMANI JAMANI SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA,NAIMBA MAHAKAMA IMTIMULIE MBALITU HUYU JAMAA,KWANI CHADEMA HAINA MTU MWINGINE WA KUMSIMASHA,TUTAMCHAGUA HATA KAMA NI JIWEAU NYAU,AU BUNDI,LAKINI LEMA HAPANAAAAAA

    ReplyDelete
  15. MKUBWA UMENENA HAPO,LEMA NI JANGA NDUGU ZANGU,AMECHANGIA SANA KUVURUGA AMANI YETU HAPA A.TOWN,ILA TUSISAHAU KUWA EDUCATION MATTERS,LEMA HAPANAAAAAAAAAAAAAAAAAAA,TUMESEMA WANA ARUSHA,TUMUOGOPE KAMA UKOMA

    ReplyDelete
  16. maneno hayo,sio arusha tu tz yote tusema lema hapanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,alipewa cheo kashindwa kutumia,mbowe tupeni hata vicent nyerere,makamda oyeeeeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  17. Nikweli Babu anakadi ya CCM lakin hamzuii kutetea maslai ya Nchi.Na maneno yote haya ni kwasababu CCM imekalia kuti kavu.."CCM tayari mmesha haribu angaliane mnajipanga vipi na sio maneno ya sio na mantiki yoyote..

    ReplyDelete