13 December 2012
Wawili wafariki katika matukio tofauti Dar
Na Leah Daudi
WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti yaliyotokea jijini Dar es Salaam, likiwemo la maiti ya mtoto mchanga kuokotwa ikiwa imeviringishwe katika kanga.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Mariaetha Komba, alisema tukio la kwanza ni la maiti ya mtoto mchanga kuokotwa kwenye eneo la Majohe, katika machimbo ya mchanga.
Alisema mtoto huyo wa jinsia ya kike ambaye alitupwa na mtu asijefahamika, anakadiriwa kuwa na umri wa wiki mbili ambapo katika uchunguzi wa awali, wamebaini kanga iliyotumika kumviringisha mtoto huyo iliandikwa Julieth Godwin,
wakiamini jina hilo ni la mama mzazi wa mtoto.
“Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Amana, juhudi
za kumtafuta mama mzazi wa mtoto zinaendelea,” alisema.
Wakati huo huo, mwanaume ambaye hakufahamika jina lake ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30, amekutwa amekufa baada ya kutapika damu nyingi.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Engelbet Kiondo,
alisema maiti hiyo ilikutwa juzi saa 4 asubuhi, eneo la Mbagala Mzambarauni.
Alisema chanzo cha kifo chake hakijafahamika ambapo mwili wa marehemu ulikutwa hauna jeraha lolote. Maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke kwa uchunguzi zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment