04 December 2012
Watakiwa kuchangia huduma za Zimamoto
Na Neema Kalaliche
WITO umetolewa kwa waananchi kuona umuhimu wa kuchangia ada ya ukaguzi wa tahadhari na kinga ya moto katika majengo na maeneo mbalimbali ili Jeshi la Zimamoto liweze kufanya kazi
kwa ufanisi na kutoa huduma zake kwa wakati.
Mkaguzi Msaidizi wa jeshi hilo, Elia Kakwembe, aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika mafunzo ya tahadhari na kinga ya moto yaliyoendeshwa na wataalamu kutoka Humburg nchini Ujerumani.
Alisema huduma za zimamoto zinapaswa kuwepo wakati wote
kwa wananchi hivyo aliwaomba wachangia ada hiyo ili wafanye
kazi pamoja.
Kwa upande wake, Mkaguzi Msaidizi ambaye ni Kamanda wa Operesheni Mkoa wa Kinondoni, Joseph Mwasabeja, alisema kitendo cha Jeshi la Zimamoto kutofika kwa wakati kwenye
majanga ya moto husababishwa na madereva wa daladala
kukataa kuwapisha wanapokuwa barabarani.
“Baadhi ya madereva daladala wanaposikia sauti ya king'ora cha zimamoto hawataki kutupisha ili tuweze kuwahi katika majanga ya moto hivyo kusababisha tuchelewe,” alisema.
Alisema mwaka huu wa fedha, wameanza kujenga Kituo cha Lugalo ambacho kikikamilika kitakuwa na gari la zimamoto na wagonjwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment