Na Severin Blasio, Morogoro
ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Morogoro, Bw. Abeli Ruanda pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Morogoro Bw. Rajabu Ally ’Kiselengo’, wametangaza rasmi kuhamia CCM.
Mbali ya viongozi hao, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Mkundi, Bw. Said Athumani, naye alitangaza kukihama chama hicho na kuhamia CCM, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shujaa mjini humo.
Wakizungumzia na gazeti hili kwa nyakati tofauti, viongozi hao walidai kujiunga upinzani kwa bahati mbaya kama abilia awapo barabarani ambapo linapotekea gari lenye umbo na rangi nzuri hulazimika kuingia ukiamini ni chombo imara wakati mashine
yake ni mbovu na haiwezi kuwafikisha popote.
Mbali na kuipongeza CCM kwa uimara wake, viongozi hao walisema vyama vya upinzani havina sera ya kuwakomboa Watanzania bali viongozi wake wanataka kujinufaisha.
Bw. Athumani alisema ameamua kurudi CCM baada ya kubaini kuwa, CUF kimekufa ambapo hivi sasa kinasukumwa na chama tawala ambacho ndio chenye sera zinazotekelezeka.
Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Bw. Innocent Kalogelis, alitoa mwezi mmoja kutatuliwa mgogoro unaofukuta chini chini kati ya viongozi wa chama hicho na kuwataka wakae mezani kumaliza tofauti zao na kuchochea maendeleo ya wannchi.
“Hatukubali wapiga kura wetu waendelee kushumbuliwa na Serikali kwa kukosa eneo la kufanyia biashara…mapendekezo yangu eneo la wafanyabishara wa Mahindi ziwekwe biashara za jioni ili akina mama watafute riziki na halamashauri ikusanye kodi,” alisema.
No comments:
Post a Comment