18 December 2012
Prof. Lipumba: Mafisadi CCM wamefanikiwa
Na Rehema Maigala
MWENYEKI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema mtandao wa mafisadi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), umefanikiwa kupata uongozi kwa asilimia
75 na mikakati waliyonayo ni kuchukua nchi ifikapo 2015.
Prof. Lipumba aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la chama hicho ambao wajumbe walijadili mambo 11 ya msingi.
Alisema chaguzi mbalimbali za CCM zilizofanyika hivi karibuni, zilitawaliwa na vitendo vya rushwa kwa wagombea wasioa na sifa za kuwa viongozi na wenye masilahi binafsi badala ya chama.
“Chaguzi za CCM zilitawaliwa na rushwa hasa wa wanawake, mafisadi wasipewe nafasi ya kuongoza nchi na safari hii, hatuta kubali wachaguliwe viongozi wenye masilahi binafsi,” alisema.
Alisema Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, naye aliwahi kulalamikia vitendo
vya rushwa ndani ya chama na kusisitiza kama mgombe haba pesa, hawezi kushinda nafasi ya Halmashauri Kuu (NEC).
“Gharama za maisha zimepanda, elimu imeshuka na kusababisha Watanzania waishi bila ya matumaini katika nchi yao, Tanzania hakuna mwananchi anayepata haki kama binadamu,” alisema.
Akitolea mfano wa Shekhe Ponda Issa Ponda na kudai hadi sasa amenyimwa dhamana wakati kisheria kesi yake alistahili kuipata lakini hadi sasa anaendelea kusota rumande.
Prof. Lipumba alilalamikia muda mchache waliopewa wananchi kutoa maoni ya Katiba Mpya tofauti na wanavyofanya katika nchi zingine ambazo hutoa muda wa mwaka mmoja kama Kenya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
NI VEMA CHAMA CHA CUF KISHUGHULIKIE UMOJA NA UTENGAMANO NDANI YA CHAMA CHAO NA KIANZE SAFARI YA KUELEKEA KWENYE DEMOKRASIA KWA KACHANA NA UDIKTETA KWA KUFANYA UCHAGUZI HURU NA WA HAKI KUANZIA NGAZI YA KATA HADI TAIFA SI VEMA KUSEMA MAVI YAKO YANANUKIA ILA YA WENZAKO YANANUKA WATUDHIHIRISHIE KUWA KWAO RUSHWA HAITUMIKI KWA VITENDO
ReplyDelete