13 December 2012
Mwalimu anusurika kuuawa akituhumiwa uchawi
Na Theonestina Juma, Kagera
MWALIMU wa Shule ya Msingi Kashai, iliyopo Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, Bi. Benedetha Katabaro (56), ameokolewa na polisi waliolazimika kutumia mabomu na risasi za moto baada ya wananchi kuzingira nyumba yake ili kutaka kumuua na kuichoma moto wakimtuhumu kuwa ni mchawi.
Shughuli za maendeleo kwa wakazi wa eno la Majengo analoishi Bw. Katabaro, zilisimama tangu juzi usiku hadi jana mchana kutokana na vurufu zilizokuwa zikifanywa na waananchi.
Bw. Katabaro anatuhumiwa kuwahifadhi watoto sita na kuwafanya msukule ambapo kaka wa mwalimu huyo, Bw. Rwezahura Bonny (63) ambaye ni mfanyabiashara nchini Rwanda, alisema tuhuma
hizo zimechangiwa na migogoro ya kifamilia.
Alisema Desemba 10 mwaka huu, mdogo wao wa kike anayeitwa Bi. Benedicta Bukende, alifika nyumbani kwa mtuhumiwa ambaye ni dada yake akitoka Kamachumu Muleba akiwa na watoto wake wawili ili kwenda kumpumzika.
Aliongeza kuwa, Bi. Bukende alipata matatizo ya kufiwa na mumewe jijini Dar es Salaam, (Kanali Bukende), ambaye
alizikwa Kamachumu hivi karibuni.
“Mke wa marehemu alikwenda kwa dada yake ili aweze kupumzika kwa siku tatu baada ya kupewa mapumziko, upande wa mumewe haukufurahishwa na uamuzi huo kwani wao walimtaka mjane msibani siku tisa ili kukamilisha baadhi ya mambo ya mila.
“Alipofika nyumbani kwa dada yake, ndugu wa mume walikwenda Kituo cha Polisi Kamachumu kutoa taarifa juu ya kuibiwa watoto wao na mama yao ambaye ni mke wa marehemu, baadhi ya wifi zake na mjane walifika Kashai kwa Bw. Katabaro wakiambatana
na baadhi ya askari,” alisema Bw. Bonny.
Aliongeza kuwa, wakati huo Bw. Katabaro alikuwa shuleni hivyo alifuatwa ambapo hali hiyo ilimshtua mwalimu huyo na wenzake, hivyo baada ya kurudi nyumbani, kati ya watoto hao wawili ambao walikuwepo nyumbani.
Alisema mtoto mmoja wa marehemu anayeitwa Gloria Bukende (21), inadaiwa ana tatizo la akili na hawezi kuzungumza vizuri
ambapo ndugu zake wanafahamu hilo lakini kwa kuwa mawifi
walishindwa kuelewena na mke wa marehemu, walianza
kurushiana maneno na kutuhumiana uchawi.
Maneno hayo yalivuta hisia za wananchi na kuanza kuenea mji nzima juu ya mwalimu huyo kutuhumiwa kumuweka mtoto msukule ambapo mke wa marehemu alilazimika kurudi Kamachumu pamoja na watoto wake wawili Gloria na Denis.
Bw. Bonny alilazimika kurejea nchini baada ya kusikia kifo cha shemeji yake na kusisitiza kuwa, katika familia hiyo hawana
ugomvi wowote ila alishangaa kusikia mambo yanayoibuka.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ilifika eneo la tukio, saa tatu asubuhi ikoongozwa na Mwenyekiti Mkuu wa Wilaya Bi. Ziporah Pangani, alishindwa kuhutubia mamia ya wananchi waliofika eneo hilo ambao walikuwa wakikumzoea ambapo kutokana na hali hiyo, polisi walilazimika kutumia mabomu
ya machozi kuwatawanya wananchi ambao nao walikuwa
wakirusha mawe kupambana nao.
Serikali ililazimika kuhamisha vifaa vya mwalimu huyo kwa
kutumia gari lenye namba ya sajili T 516 AAW, aina ya Fuso
na kuvipeleka kusikojulikana.
Akizungumza na gazeti hili, Bi. Pangani alisema tatizo lililotokea katika eneo hilo si la kishirikana kama inavyodaiwa bali ni fitina zilizojaa uchonganishi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tatizo watu hawamjui Mungu, amjuaye mchawi lazima nae awe mchawi.neno la MUNGU linasem vita yetu si juu ya damu na nyama bali ni juu ya mamlaka na wakuu wa giza, yaani vita ya kiroho ie we fight spiritual entities not fresh and blood, when you fight body and fresh you fight a wrong battle and you cannot win the battle.Balumuna bange tujifunze hekima hii ya kimungu ndo itatusaidia.Am Ladislaus mwanza.
ReplyDeleteILA TANZANIA KIMATAIFA ILISHINDA MEDALI YA DHAHABU KATIKA USHIRIKINA NA DUNIA INAFAHAMU HIVI NATUMAINI NDIO WANAOTUMIA FEDHA NYINGI ZA KIGENI KWENDA KUOMBEWA NA T.B. JSHUA HUKO NIGERIA
ReplyDelete