04 December 2012
Mnyika kuwasilisha hoja binafsi
Na Rehema Maigala
MBUNGE wa Ubungo, Bw. John Mnyika (CHADEMA), leo anatarajia kuwasilisha hoja binafsi juu ya Serikali kuchukua hatua
za haraka kuboresha upatikanaji wa maji safi na uondoaji maji taka jimboni humo na jijini Dar es Salaam.
Hoja hiyo ataiwasilisha kwa uongozi wa halmashauri ya jiji hilo ili iweze kujadiliwa na madiwani na kupitisha azimio la kuchukuliwa hatua za haraka kuboresha huduma hizo.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana katika vyombo vya habari, ambayo imesainiwa na Katibu Msaidizi wa ofisi yake, Bw. Aziz Himbula, alisema Bw. Mnyika ameamua kuchukua hatua hiyo ili halmashauri itimize wajibu wake wakati akisubiri kuwasilisha
hoja binafsi bungeni Februari 2013.
Alisema Serikali kupitia kwa Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, Novemba 7 mwaka huu, akiwa bungeni mjini Dodoma alitoa kauli iliyohusu mpango maalumu wa kutatua matatizo ya maji katika jiji la Dar es Salaam.
Bw. Himbula alisema baada ya kauli hiyo, Bw. Mnyika alisimama na kuomba mwongozo wa spika kwani kauli hiyo haikuwa sahihi na haikuweka msingi kamili juu ya utatuzi wa tatizo hilo kwa haraka.
“Katika kufuatilia masuala ya maji, Bw. Mnyika alianza kwa kufanya kongamano la maji jimboni mwanzoni mwa mwaka
2011 ili kukutanisha wananchi, mamlaka husika na wadau wengine ili kupata ufumbuzi wa tatizo hili,” alisema.
Oktoba mwaka huu, Waziri wa Maji Prof. Maghembe alifika jimboni humo na kuzindua visima katika Kata za Saranga na
Kimara isipokuwa maeneo ya Mbezi Malambamawili.
Alisema maji ya visima yamebainika kuwa na chumvi nyingi hivyo aliahidi kutafuta ufumbuzi hususan katika eneo la Msuguri na Msingwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment