04 December 2012

Daladala 308 zakamatwa, kutozwa faini


Na Grace Ndossa

MAMLAKA ya Udhibiti, Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imeanza oparesheni kuzikamata daladala zinazokatisha ruti nyakati za jioni.

Daladala hizo ni zile zinazofanya safari zake kati ya Mwenge, Tegeta hadi Bunju. Ofisa Mfawidhi wa SUMATWA Kanda ya Mashariki, Bw. Konradi Shio, aliyasema hayo Dar es Salaam
jana wakati akizungumza na gazeti hili.

Alisema lipo tatizo la magari mengi kukatisha ruti hasa nyakati
za jioni hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa abiria.

“Katika oparesheni hii, SUMATRA inashirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani kuzibaini daladala zinazokatisha ruti na kuyafungia kwa muda wa mwezi mmoja,” alisema.

Aliongeza kuwa, operesheni hiyo ilianza Novemba 8 mwaka huu na wameweza kukamata daladala 308, ambazo zimepigwa fani ya sh. 250,000.

“Daladala 42 zimefungiwa kwa muda wa mwezi mmoja na wamiliki wake wametakiwa kuleta mikataba ya madereva wengine,” alisema.

No comments:

Post a Comment