10 December 2012

Marais SADC kuhudhuria miaka 51 ya Uhuru Dar


Na Rehema Maigala

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Meck Sadick, amesema maadhimishi ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara yanatarajiwa kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Marais wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Maadhimisho hayo yatafanyika Dar es Salaam kesho katika Uwanja wa Uhuru kuanzia saa 12 asubuhi, ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.

Alisema katika kipindi cha miaka 51 ya uhuru, Tanzania imepata mafanikio makubwa ya kujivunia katika nyanja za uchumi, ulinzi, usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa.

“Kutokana na maendeleo yaliyopatikana, kauli mbiu ya maadhimisho haya inasema 'Uwajibakaji, Uadilifu na Uzalendo
ni Nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu,” alisema Bw. Sadick.

Aliongeza kuwa, wamiliki wa vyombo vya usafiri (daladala), wanaruhusiwa kupeleka abiria uwanjani kuanzia asubuhi na kuwaomba wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi.

Katika maadhimisho hayo, kutakuwa na burudani maalumu ambayo itatolewa na Kundi la Taifa la Sanaa nchini Rwanda, ngoma za asili kutoka Ukerewe, Dodoma na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment