10 December 2012
Kadi ya CCM yamponza Slaa *Sasa ashinikizwa kujiuzulu nafasi yake *Wanachama wadai kukosa imani naye
Na Mwandishi Wetu
MJUMBE wa Mkutano Mkuu Taifa CHADEMA, mkoani Mbeya, Bw. Edo Mwamalala, amemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Willibrod Slaa, kujiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kikidhalilisha chama chao kwa kuendelea kumiliki kadi ya CCM.
Bw. Mwamalala aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea jinsi alivyoguswa
na kitendo cha Dkt. Slaa kukiri hadharani kumiliki kadi ya CCM wakati anajua dhamana kubwa aliyopewa katika chama hicho.
Alisema katiba ya chama hicho sura ya tano, ibara ya kwanza kifungu kidogo cha sita 5.1.6 kinachosema, mwanachama wa
chama hicho hapaswi kuwa mwanachama wa chama kingine
cha siasa baada ya kujiunga CHADEMA.
Alisema Dkt. Slaa ameanza kuwapa mashaka wanachama wa chama hicho na wengine kuamini huenda huenda yupo CHADEMA kwa kama kibaraka wa CCM anayetumiwa kwa mambo mbalimbali.
“Hivi karibuni Dkt. Slaa amekiri kumiliki kadi ya CCM na kudai kuitunza kama kumbukumbu, halii hii inaonesha bado anatumukia vyama viwili vya siasa kwa maana ya CCM na CHADEMA.
“Umefika wakati wa kiongozi huyu kuwajibishwa na chama, katika mfumo wa vyama vingi, kiongozi wa chama lazima awe mfano kwa wengine hivyo kitendo hiki kinaleta mashaka makubwa,” alisema.
Alimtaka Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Freeman Mbowe, kuchukua hatua badala ya kuliacha jambo hilo hewani na kama atashindwa kulishughulikia, viongozi wengi zaidi ndani ya chama hicho wanaweza kujitokeza na kusema wanamiliki kadi za CCM.
“Hili ni jambo la hatari sana, wanachama wataamini chama chetu kinaendeshwa na vibaraka wa CCM, haiwezekani Katibu Mkuu wa chama awe anamiliki kadi ya chama tawala.
“Wapo ambao watajitokeza kunikejeli na kudai nimetumwa lakini mfumo wa demokrasia, unatoa fursa kwa kila mtu kueleza kile anachokiona ili kujenga siasa bora nchini,” alisema.
Alisema Dkt. Slaa amekosa uadilifu, sifa za kukitumikia chama hicho na kuongeza kuwa yupo tayari kuchukiwa kwa kueleza
ukweli wa kile anachokiamini kama mwanachama.
Bw. Mwamalala alisema kama chama hicho kitashindwa kuchukua hatua zozote, atapeleka hoja binafsi katika Mkutano Mkuu kutaka Dkt. Slaa ajadiliwe na kuchukuliwa hatua.
“Wakati Dkt. Slaa anondoka CCM, alipaswa kuwaachia kadi yao, sisi wenye mapenzi mema na CHADEMA, hatuko tayari kuona tunaishi ndani na kadi ya chama ambacho tunataka kukiondoa madarakani katika Uchaguzi Mkuu 2015,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
haya bwana!
ReplyDeleteyou are not a person 2 be followed as to what u did
ReplyDeleteAcheni uzumbukuku! Kwani walioweka kumbukumbu ya matanuru yaliyotumiwa na wajerumani kuchomea waisraeli nao ni wakatili kama Hitler? Kumbukumbu ni jambo la muhimu hata kama kinachokumbukwa ni kitu kiovu au kibaya! Wengi tunakadi za TANU Youth League, TANU na CCM lakini ilikuwa Youth League, TANU na CCM ya enzi hizo ilipokuwa inatetea maslahi ya wanyonge! Kuna ubaya gani kuweka kumbukumbu yake? Hii ni cheap propaganda style ya Nauye feki! Hakika kama Nauye, Wahasira na CCM wanaona hii ndiyo style ya kujikwamua toka tope basi CCM imeishiwa mbinu! Mbona wao wamempokea Wasira pamoja na kwamba alikuwa NCCR? Wanajuaje alirudisha kadi? Hata kama hakurudisha, kuna tatizo gani? Acheni propoganda zilizopitwa na wakati. Sie tunataka kusikia Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi, mafisadi wanaenda Segerea baada ya kufilisiwa, matumizi ya serikali yanapungua, elimu na matibabu bure, maji safi na salama kwa wote, ajira kwa kila kijana, polisi wanaacha kuua raia, polisi waliouwa wanapelekwa kwa pilato, migodi inarudishwa mikononi mwa serikali, zeru zeru wanaacha kuaawa, watu wanaacha kuchunwa ngozi, watoto wote wanakalia madawati badala ya mawe, n.k. Upuuzi wenu bakini nao ndani ya NEC au CC!
ReplyDeleteni kweli ndg yangu.ukiona hivyo ujue hata maana ya kumbukumbu kwa huyo anayemtaka slaa ajiuzulu hajui
Deletekaka umenisaidia sana bwana. upuuzi wa ccm unaoneakana wazi kaboisa asante sana
Deleteni kweli aonyeshe ushujaa wa kuji
ReplyDeleteuzulu
Kwa kiongozi wa juu katika chama cha CHADEMA, ilibidi aonyeshe mfano mzuri kwa wanachama wake. Mbona wakiwa kwenye mikutano yao ya hadahara wanawahimiza watu wanaotoka vyama vingine kujiunga na CHADEMA wawasilishe kadi za chama wanakotoka na kuzikabidhi kwa uongozi mbele ya halaiki?. Sasa iweje Dr. Slaa, aendelee kukaa na kadi ya CCM wakati yeye mwenyewe kwa hiari yake aliamua kujitoa CCM baada ya jina lake kutopendekezwa kugombea uchaguzi kwenye chama hicho tawala? Jamani nyini wanasiasa, acheni kutudanganya, mnachotafuta ni maslahi binafsi wala sio kutetea wanyonge wa nchi hii... LEAD BY EXAMPLE MY DEAR BROTHER
ReplyDeleteKadi ya zamani inaathari gani kwa chama? Si kumbukumbu zake tu? Hujui kama ile kadi ni mali yake binafsi?
ReplyDeleteTuanaacha kujadili mambo ya msingi tunajadili personal property za mtu mmoja.
Unaonekana huwezi kupambanua mambo, kwa kukaa na kadi anaongeza idadi ya wanachama wa Chama chenye kadi hiyo.
Deletenampongeza bw.slaa kua mkweli kwamba yeye c.chademaaaaa
ReplyDeleteNdugu yangu Edo, logic hapa ndogo. Wala usikauke mate mdogo wangu.Nenda kwa katibu Mkuu wa CCM au Kwa shoga yako Nape akwambie kama Dr Slaa ni mwnachama HAI wa CCM ndipo uje na hoja hiyo. Mwanachama wa chama cha siasa lazima atimize masharti ikiwemo kulipia ada ya uanachama wa chama husika.
ReplyDeleteHata Nape akibaki na chati lake la kijani, lakini akasema ni ufisadi wabunge kuchukua posho za vikao, akawa tayari kupinga kwa vitendo tume ya uchaguzi kwani sio huru, Akasimama na kusema mbele ya bosi wake kuwa Jeshi la police linafanya kazi ya siasa kwa mifano iliyowazi sisi hatuna shida naye.
Kinachokusumbua Edo ni kidogo, Jaribu kutupa mifano ya matendo ya DR Slaa yaliokaa KI CCM, tutakuunga mkono.
ACHENI UJINGA WAKATI FULANI AUGUSTINE LYATONGA MREMA ALIHAMA NCCR MAGEUZI KWENDA TLP UMAARUFU WA NCCR MAGEUZI UKAFA JARIBUNI KUFA CHADEMA KWA KUMFUKUZA DR.SLAA HICHO SIO CHAMA NI PREASURE GGOUP ILI WAFADHILI WAENDELEE KUTUPA MSAADA NI CHAMA GANI KISICHOFANYA UCHAGUZI
ReplyDeleteDuh, sikujua! Kumbe hakunaga uchaguzi?
ReplyDeletekwani shaka liko wapi basi? sisi watanzania wote tunapenda mabadiriko lakini tuliowapa dhamana ya kutufanyia mabadiliko ni ndumila kuwili! kwa mtu kama slaa akadi hiyo angaliiona kama harafu! sasa iweje haikumbatie na huwenda akawa ana itunza kuliko mali zake nyingine! kwa hiyo haingii akilini kama slaa ni pure mwanamageuzi anayeipenda nchi hii ! ninatia shaka kumshabikia na kumpa matumaini yangu ya kutupeleka mbele katika mafanikio ! kama kweli samaki moja akioza wote wameoza basi kwa uwanachama wake huo wa ccm na chavyema ! basi naye ameoza hakuna haja ya kusimama jukwaani na kusema et kuna mafisadi kifupi ni unafiki kwa kuwa huwezi imba wimbo usio ujua!
ReplyDeletemakamanda kuen wapole,Dr. c CCM , chekin kaz anayoipiga yaan kila kunapokucha yupo mzigon kwa ajili ya taifa hili, hiyo ni kumb2 yake tu kama alivyokili. Hicho kicwe kgezo cha makamanda kuvunjika moyo. NEVER GIVE UP
ReplyDeletedu? mbona nina kadi ya TANU nirudishe kwa nani?
ReplyDeleteKwani Dr. Slaa alitakiwa airudishe kadi ya CCM kwa nani? Mkitoka katika chama fulani kadi hamtakiwi kuwarudishia wenye chama bali ukipenda unaikabidhi kwa viongozi wa chama chako kipya iikuthibitisha kuwa umehama, lakini siyo lazima kufanya hivyo. Tanzania tuna utamaduni wa kuhama vyama na haimlazimishi yeyote kurejesha kadi. unapofukuzwa uanachama kwa makosa au kukiuka taratibu za chama husika ndipo unapobanwa kukabidhi kadi yako. Wapo viongozi wengi ndani ya CCM wana kadi za vyama vya upinzani kila mmoja kwa sababu zake lakini bado wao ni CCM
ReplyDeletejamani Watanzania wenzangu achaneni na mambo madogomadogo, shughulikieni kuweka hatima ya maisha yenu kwenye mikono salama. jadilini mikakati ya kujikwamua na hali ngumu ya maisha, kuwakabili wanaosababisha maisha hayo kuwa magumu na chama kinachokumbatia wahujumu hao kwa propaganda zakuchunguza maisha ya mtu badala ya kuinua hali ya watu.muwe na mawazo mazito badala ya mepesi mepesi yanayozungumzia kuwa na kadi,sijui kutukanana,kuandi ka matusi badala ya kuchangia mambo yanayoleta tija.HAKUNA SIRI KUWA WATAWALA WANATUMIA FURSA KAMA HIZI KUTOA WATU KATIKA UHALISIA NA KUSHUGHULISHA MAWAZO YETU KUJIDILI UPUUZI, TUSIKUBALI BADALA YAKE TUJIULIZE KAMA BADO WANAJICHAGUA KWA RUSHWA JE HAKI ITATENDEKA NCHINI, JE ,VIONGOZI WALIO ZAO LA KURA ZA RUSHWA WATAKABILI RUSHWA? NA JE NYUMBA ZA UMMA WALIZOGAWANA KAMA HAZINA WENYEWE NA VIWANJA VIKUBWA VINAVYOZUNGUKA NYUMBA HIZO WALIZO CHUKUA KWA BEI YA KUTUPA WATAENDELEA KUKAAMO BILA KUHOJIWA NI UHALALI GANI AU HAKI GANI ILIWAPA MALI HII YA UMMA BILA KWAULIZA WENYE MALI KAMA WAKO RADHI AU VIONGOZI NDIO WANANCHI TU;HIVI TUNAJALI MAFISADI NA WAHUJUMU WA VIWANDA VYETU WALIVYOVIUA NA KUJIMILIKISHA MAENEO NA MITAMBO,WANAOIBA FEDHA ZETU NA KUZIHIFADHI N'GAMBO HUKU TUKIWASAKAMA WALE WANAOTUFAHAMISHA MAOVU HAYO KAMA KWAMBA WAO NDIO WABAYA WETU NA WENYE DHAMBI KUTUJULISHA MALI ZETU ZINAPOPORWA?JE WANAOTAFUNA FEDHA ZA MAENDELEO NA MIRADI KUKWAMA KATIKA HALMASHAURI ZETU KAMA HATUNA WASIMAMIZI WA RASLIMALI ZETU HIZO HATUWAONI NA BADALA YAKE TUNASHABIKIA MAMBO MADOGO KAMA MTU KUMILIKI KADI, HIYO INASAIDIAJE MTANZANIA. NAZIDI KUWAKUMBUSHA WATANZANIA TUKATAE DHANA KWAMBA HATUWEZI KUBADILI MAISHA YETU. UMASKINI ULIOPO HATUKUUMBIWA, BALI UNASABABISHWA NA TUNAGHILIBIWA KUWA WATAWALA WA SASA WATAUMALIZA, SI KWELI, HEBU TUTUMIE HAKI YETU YA KIKATIBA KUBADILI MAISHA YETU. TUSIDANGANYWE TUKAJITIA UWAZIMU WA KUTUKANANA BADALA YA KUJENGA HOJA.TUMIENI FURSA HIZI ZA KUCHANGIA MAWAZO VIZURI TUWAELIMISHE WENZETU
ReplyDeleteHaina maana kwa wanachama wanaohama CCM kwenda chadema Kurudisha kadi zao. Na Dr Slaa ndio amekuwa kiongozi wa kwanza kuomba watu warudishe kadi za CCM, kumbe yeye anajua anachofanya. BAVICHA muondoeni huyo kigeugeu.
ReplyDeletekumbe mtu akifumaniwa anakuwa na sababu kedekede,kadi kwa ukumbusho,siyo akiona kugumu anarudi tena sisiemu? Je amelipia hadi lini.Haya upinzani wa TZ aheri Mtikila na DP yake
ReplyDeleteswali: slaa aliwaambia wanachadema mapema kuwa nahamia chadema na nabaki na kadi yangu ya ccm? mbona wengine wakihamia,kitu cha kwanza ni kudhalilisha chama kwa kurudisha kadi!!
ReplyDeletekumtoa slaa si ndo chadema itakufa! ni kwamba itajichotea sifa ya kusafisha chama!
Je slaa sasa hivi akifa in maana mabadilika ( M4C)inakoma? think twice you people.
HAYA SASA KAZI NI KWENU WADAU WA UPINZANI.je ni CUF, NCCR, TLP, UDP,DP.... au CHADEMA?
ReplyDeleteCHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA!
ReplyDeleteCHADEMA 2015 hata wasemeje! kamavipi watoke waende uko ccm wanakotaka, Dr. Ni CHADEMA pure!
ReplyDeleteinamaana wale wanaovaa misalaba shingoni walishiriki kumuua yesu? au wanashangilia kifo chake? au wanavaa misalaba kama kumbukumbu tu au je aliyemuumba yesu anahisije?je majumba ya makumbusho ni yanini? mbona kuna wanyama wakali na nyoka wakubwa mno?kumiliki kadi ya chama kingine kama kumbukumbu kunatofauti gani na maswali yaliyotangulia tujichunguze sana upeo wetu wakufikiri ili tupate majibu yenye hekima na ufahamu.sawa dokta kamiliki kadi lakini m4c anayoiongoza pamoja na mikutano yake yote mbona hawatetei wenye kadi tusiangalie mapungufu machache tuangalie amekisaidiaje chama chake
ReplyDeleteCHADEMA chama kampuni ya watu binafsi. Ina mahelkopta na mashangingi kibao. Bado inachangisha wanachama kununua hisa. Mgawo 2015. duuuu. Kipeni kura tusikose mgawo
ReplyDeleteNadhani bwana Mwamalala ana shida kubwa sana katika kufikiri. Nadhani haelewei kabisa dhana wala maana ya historia. Dk Slaa kuwa na kadi ya CCM hakumaanishi usaliti hata kidogo! Historia ni historia na kamwe mtu asijaribu kuikana kwa sababu sehemu hata kama ni ndogo ama mbaya isiyopendeza, ikiachwa kuandikwa historia huwa pungufu na kwa maana nyingine hiyo haiwi historia.
ReplyDeleteNitatumia mfano hapa na kama bwana Mwamalala ni mtu mwenye uwezo na mwenye kupenda kuelewa, atajifunza jambo hapo. Historia ya dunia haiwezi kuwa kamili watu wabaya kama vile Hitler, Musolini, Stalin, Iddi Amin Dadaa na wengine waliotawala kidikteta hatatajwa. Kwa wakristo watakubaliana nami kwamba mtu hawezi kuandika historia ya wokovu bila kumtaja Shetani ambaye ndiye jamaa mbaya hata kama hapendwi. Ili historia ya wokovu iwe kamili lazima Shetani atajwe. Atatajwa tu!
Kama lengo la Mwamalala na wengine walio na mawazo kama yake wanajua kuwa Watanzania wanahutaji kuokolewa toka CCM, na kama Dk Slaa ni mpambanaji kweli kweli atapenda kuwa na kadi hiyo ya zamani ili siku itakapofika CHADEMA kuiondoa CCM madarakani, awe na ushahidi wa kuwaonesha watoto wake na wajukuu hata baada ya yeye kuondoka duniani wajue kwamba Baba, Babu Dk Slaa alipambana kuondoa chama cha siasa kilichoitwa CCM kilichokuwa na kadi yenye rangi ya kijani na alama ya nyundo na jembe na ushahidi utakuwa kadi yenyewe.
Busara ya kawaida ituwezeshe kumtathmini Dk Slaa kwa vitendo na kazi yake na sio kwa kuwa na kadi ya CCM. Niwakumbushe akina "Mwamalala" kuwa wapo pia wana-CCM ambao wanazo kadi za CCM lakini mioyo yao iko kwa CHADEMA. Acheni kumsumbua Dk Slaa kwa sababu ya uzumbukuku, ama ninyi akina "Mwamalala" ndio mnaotumiwa na CCM? Napenda kufikiri hivyo na kama sivyo basi nakubaliana na aliyesema kinachowafanya muongee bila upeo wa uchambuzi ni "uzumbukuku."
WATANZANIA TUMECHOKA KUIBIWA MALI ASILI ZETU MADINI WANYAMA POLI MIKATABA MIBOVU YA TANESCO TRL AIR TANZANIA NAINA HATA NDEGE SASA WATANZANIA MNANGANANIA KADI YA DR SLAA YA NINI? VIWANDA ALIVYOANZISHA MWL VIMEKUFAA VYOTE JE TUTAFIKA
ReplyDeleteUADILIFU NI ZAIDI YA TAALUMA DAKTARI ANAWEZA KUHITIMU VIZURI LAKINI AKIKIUKA MAADILI YA UDAKTARI ANAFUKUZWA;MWANAJESHI AWE NA TAALUMA YA KUPINDUKIA AKIWA SI MUADILIFU ATASALITI JESHI LAZIMA APIGWE CHINI NI UFINYU WA MAWAZO WA WALE WANAOMTETEA DR. SLAA NI KUDHIHIRISHA CHADEMA NI SLAA NA SLAA NI CHADEMA NI NANI ALIYETOA RUSHWA KWA MUNGU SLAA ATAISHI MILELE MUNAPOKOSA RASILIMALIWATU KWENYE CHAMA NA KUMTEGEMEA MTU MMOJA NI UPUNGUFU MKUBWA INADHIHIRISHA AUGUSTINE L.MREMA,CHEYO NA SASA SLAA MUNGU AKIWAPENDA ZAIDI KULIKO SISI AKIWACHUKUA VYAMA VINAKUFA TUACHE UFINYU WA MAWAZO HIVI LINI TANZANIA TUTAKUWA NA KUONDOKA MAVI YA SHINGO ??????????????????????
ReplyDeleteDr slaa hana tatizo . Na hawa watu wanaosema sema hovyo kama ccm. mimi naona ufahamu wao ni mdogo.
ReplyDeletePia sio wazalendo wa kweli walla hawajui wanalolitenda. Laiti wangelijua walitendalo wangeacha mara moja. Kwa upande wangu mimi nawaona wanaajenda ya siri na siyo hiyo kadi , wana mambo yao binafsi ambayo siyo ya masilahi ya chama. kwa kusema kuwa Dr Slaa hayupo peke yake haya yanatoka wapi? nafikiri kwa mtu mwelewa utajua waziwazi kuwa hivi ni vita vya kisiasa. Leo wataanza na huyu kesho yule. kwa taarifa hata mimi ninyo kadi ya ccm kuwa na kadi ya ccm hampi mtu kuwa na sifa za uanachama sifa ya uanachama ni uhai wa kadi yako ndg. hatakama akiirejesha leo hii akitaka kurudi ccm lazima aifufue kadi yake.au ajisajili upya.
Milango iko wazi kwa vyama vyote.
Mimi nikitaka kureja ccm lazima niifufue kadi yangu. nikiona garama ni kubwa natachukua mpya ndg. kwa sasa mimi ni mwanachama hai wa chadema.
na ile ya ccm nimeiweka toka mwaka 1989 kama kumbu kumbu zangu. sijailipia na sina mpango huo, Unajua kuna wakati unaweza kueleza mtu kitu akakuambia nionyeshe kidhibitisho. sijui kama mnanielewa vizuri.
Mwisho mimi naunga mkono kwa dr Slaa kuwa na kadi . Tena hilo ni jambo lake binafsi si vyema kulizungumzia sana.
Nawasihi waandishi wa habari waachane nalo kabisa.
Slaa ni tatizo bwana. Inaonyesha chadema haina watu makini wa kutosha. Waombe watu msakini kama akina magufuli wahamie huko. Ni aibu chama kitakachochukua nchi kua na mtu mmoja makini na wengine mashabiki tu. Unganikeni na cuf mpate lipumba, pia vyama vingine vipo muongezee akina mrema, mbatia nk. Hii ni nchi kubwa bwana, haijengwi kwa porojo!
DeleteKweli watanzania tunahitaji miaka milioni kumi labda kuweza kufumbua macho. Hivi hawa wanachama wa CHADEMA ambao leo wanataka katibu mkuu wao ajiuzulu eti kwa sababu anamiliki kadi ya CCM wanaelewa wanachofanya?
ReplyDeleteTanzania ilikuwa nchi ya chama kimoja yaani TANU kisha CCM.Kwa mwenye akili timilifu hawezi kuhoji umiliki wa kadi ya CCM kwa mtu mwenye umri kama Slaa. Kuna njia nyingi za mtu kuikna CCM aidha kuitupa kadio au kuirudisha kama wanavyotaka wao afanye au kuihifadhi kama kumbukumbu.
Nataka niwaulize hivi ukiacha kazi mahali ni lazima urudishe barua ya ajira uliyopewa na mwajiri wako?
Kama hiyo haitoshi nani ambaye anamwacha mkewe huwa anafanya sherehe kama siku ya Harusi? au kumwalika padri, mchungaji au shekhe au hta mshenga kushuhudia kuachana kwao?
Kubwa zaidi hawa wanaodai hawana imani na Slaa leo walingoja mpaka Nape awajulishe kuwa Dk. Slaa anamiliki kadi ya CCM?
Kwa mtazamo wangu hwa ni wale wale ambao ukiwapa kitu kidogo wako tayari kuchoma nyumba wanayoishi kwa imani kuwa wanaweza kujenga nyingine.
Leo slaa je wanajua pia hata Mtei ambae al;iwahi kuwa waziri ndani ya CCM kama karejesha kadi wakati wake?
Mimi naona swala la kadi ya CCM sio ajenda muhimu kwa sasa kwa kiopngozi wa BAVICHA ambaye kwa walio wengi wanadhani kuwa vijana wanakuwa na mtazamo chanya zaid