04 December 2012
Mahindi, karanga vyanzo vya saratani-TFDA
Na Heri Shaaban
MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini (TFDA), imesema
vyakula aina ya mahindi, karanga na mazao ya wanyama vinasababisha magonjwa ya saratani ya ini.
Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Bw. Hiti Silo, aliyasema hayo katika semina maalumu iliyolenga kujadili matumizi ya vyakula ambayo ilishirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wa kilimo.
Alisema utafiti uliofanywa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine, mkoani Morogoro na Chuo Kikuu cha Ubelgiji, umebaini vyakula hivyo vinachangia ugonjwa huo.
“Tafiti zilizofanywa na wataalamu katika mimea kuanzia 2010 zimebaini kwa kiasi kikubwa sumu ya ugonjwa huu inapatikana katika vyakula hivi kutokana na wakulima kuvuna vyakula vyao
na kuvihifadhi hivyo kupata ukungu,” alisema Bw. Silo.
Aliwataka wakulima baada kumaliza kuvuna vyakula, wavikaushe ili visipate ukungu ambao utasababisha walaji kupatwa na saratani ya ini.
Aliongeza kuwa, awali walifanya utafiti katika baadhi ya mikoa nchini ikiwemo Kirimanjaro, Morogoro, Mbeya, Manyara na kubaini tatizo hilo.
Alisema baada ya semina hiyo ya siku mbili kumalizika, watatoa maazimio ya pamoja ili yakatumiwe na wakulima mbalimbali kwa ajili ya tahadhari.
Kwa upande wake, Naibu Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Donald Mbando, alisema kazi kubwa ya TFDA ni kupima usalama wa vyakula ili kulinda afya za jamii.
Alisema lengo la semina hiyo ni kutoa elimu kwa jamii ili ifahamu madhara yanayoletwa na kansa ya ini kutokana na vyakula waweze kuchukua tahadhari.
“Tunatafuta mbinu ya kutoa elimu kwa umma ili fangasi wasiingie katika vyakula baada kuvunwa kutoka shambani,” alisema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment