18 December 2012
Jumuiya yaiomba serikali itoe mapumziko
Na Stella Aron
JUMUIYA ya Istiqaama tawi la Tanzania, imeiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuweka mapumziko katika siku ya
maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu.
Akizungumza na Majira, Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Alhad Mussa Salum, alisema anaungana na jumuiya hiyo kwa kuiomba Serikali iitambue siku hiyo na kuifanya iwe ya
mapunziko kama zilivyo sikukuu nyingine.
“Naungana na jumuiya hii kuiomba Serikali itambue umuhimu
wa Mwaka Mpya wa Kiislamu na kukubali kuweka mapumziko, Waislamu nao wanapaswa kutumia kalenda ya Kiislamu katika shughuli zao mbalimbali,” alisema.
Aliongeza kuwa, Serikali ina nafasi ya kutambua umuhimu wa siku hiyo na kuwalipa watumishi wa misikiti kwa kutumia kalenda hiyo na kusisitiza kuwa ni jambo la kushangaza kwa baadhi ya taasisi za Kiislamu kushindwa kufuata tarehe hizo.
“Bado kuna changamoto kubwa kwa Waislamu juu ya kutumia kalenda ya Kiislamu, ufike wakati kila Muislamu awe na kalenda ambayo itamsaidia katika mambo mengi ya dini yetu,” alisema.
Mwenyekiti wa Vijana jumuiya hiyo, tawi la Dar es Salaam, Bw. Salehe Salahe, alisema kwa muda mrefu waniomba Serikali itambue umuhimu wa siku hiyo na kukubali iwe ya mapumziko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment