Na Stella Aron
RAIS Jakaya Kikwete, leo atazindua na kukabidhi nyumba 36 za waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto zilizojengwa eneo la Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.
Taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Meck Sadiki, ilisema mbali ya uzinduzi huo, Rais Kikwete pia atakabidhiwa majengo ya huduma za mama
na mtoto katika Hospitali za Mnazi Mmoja, Sinza, Rangi Tatu na Balozi wa Korea Kusini kwa niaba ya raia wa nchi hiyo.
Alisema makabidhiano ya nyumba hizo yatafanyika kuanzia saa nane mchana hadi 10 jioni na kuwaomba wananchi mbalimbali kuhudhuria shughuli hiyo.
“Hafla ya kukabidhi majengo ya huduma za mama na mtoto, itaanza saa 2:30 hadi saa tano asubuhi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Baada ya hapo atakwenda Hospitali ya Sinza iliyopo wilayani Kinondoni, hadi saa saba mchana na kumalizia Hospitali ya Rangi Tatu iliyopo Temeke hadi saa tisa alasiri.
No comments:
Post a Comment