13 December 2012
Elimu ya ugonjwa wa saratani itolewe kwa wananchi
UGONJWA wa saratani ya shingo ya kizazi nchini, huwashika hasa wanawake wenye umri kati ya miaka 25-50 tofauti na saratani nyingine ambazo huweza kuwapata watu wa jinsia zote.
Wanawake wengi nchini wanaobainika kuugua ugonjwa huo kila mwaka katika nchi zinazoendelea ni asilimia 80. Asilimia 60 ya wagonjwa wanaofika kupata matibabu katika Taasisi ya Saratani
ya Ccean Road ya jijini Dar es Salaam, wanaugua ugonjwa huu.
Utafiti wa kitabibu unaonesha kuwa, ugonjwa huo unaweza kutibika na mgonjwa kupona kabisa kama wagonjwa husika, watakwenda hospitali mapema ili kufanyiwa uchunguzi na kuanza matibabu.
Saratani ya shingo ya kizazi ni mabadiliko ya chembechembe hai zilizopo juu au zinazofanana na shingo ya uzazi na kuchukua
miaka 15 hadi kugundulika kwake.
Wataalamu wanasema kuwa, kabla ugonjwa huo haujajitokeza, kama mgonjwa atafanyiwa uchunguzi na kujulikana mapema
upo uwezekano mkubwa wa kupona kabisa.
Inaelezwa kuwa, yapo baadhi ya mambo ambayo yameonekana kusababisha ugonjwa huo kwa wanawake. Uchunguzi uliofanyika katika nchi mbalimbali duniani, umebaini ugonjwa huo unaweza kusabbishwa na vitendo vya ngono katika umri wa miaka 18.
Sababu nyingine ni uhusiano wa kimapenzi na kubeba mimba nyingi katika umri mdogo chini ya miaka 18 ambapo watoto wengi wa umri huo, huzaliwa wakiwa na maradhi hayo.
Unywaji wa pombe kupindukia pia ni moja ya sbabu inayochangia kupata ugonjwa sataratani hiyo ambapo waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI, pia wapo hatarini kupata maradhi hayo.
Sisi tunasema kuwa, ugonjwa hu o ni hatari sana hasa kwa wanawake hivyo ni vyema Serikali ikaweke msukumo katika mapambano.
Serikali inapaswa kuhakikisha elimu ya ugonjwa huo inatolewa kwa wanawake na wanaume katika maeneo mbalimbali nchini ili waweze kufahamu dalili zake na kupatiwa matibabu mapema.
Elimu hiyo itolewe kwa uwazi ili iwe rahasi kwa wananchi wote kuelewa dalili zake na kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha watoto wote wa jinsia ya kike wanaozaliwa, wanapatiwa chanjo inayotolewa kwa watoto ambao hajaanza kujihusisha na mapenzi.
Ni jukumu la kila mwananchi kushirikiana na Serikali ili kutokomeza ugonjwa huo ambao umeathiri familia nyingi
kwa kuziacha yatima na kupoteza kiasi kikubwa fedha
kwa ajili ya tiba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment