10 December 2012
Ajali mbaya yaua, kujeruhi watu 11
Na Rashid Mkwinda, Mbeya
AJALI mbaya iliyosababisha magari matatu iliyotokea jana katika eneo la Nzovwe, jijini Mbeya, imesababisha kifo cha mtu mmoja
na wengine 11 kujeruhiwa vibaya.
Chanzo cha ajali hiyo ni baada ya lori aina ya Leyland lenye namba za usajili T 721 BVD na trela lake lenye namba T 668 BGZ, kufeli breki na kuzigonga kwa nyuma daladala mbili aina ya hiace ambazo zinafanya safari zake kati ya Mwanjelwa na Tazara.
Wakizungumza na gazeti hili, mashuhuda wa ajali hiyo walisema Hiace zilizogongwa na lori hilo moja ilikuwa na mamba za usajili
T 945 AFG na nyingine T 150 AJL, ambazo zote zilikuwa zimesimama zikishusha abiria eneo la Kalobe.
“Nililiona lori hili likishuka katika barabara ya Zambia kwa mwendo kasi na lilipofika eneo la Nzovwe, likaigonga Hiace
moja kwa nyumba ambayo ilipinduka upande wa kushoto na
kuigonga nyingine ambayo nayo ilipinduka,” alisema shuhuda
wa tukio hilo Bw. Maimuna Abdallah.
Mwandishi wetu aliwashuhudia majeruhi wakipatiwa huduma za matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya ambapo baadhi yao wamelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi.
“Tumepokea majeruhi 11, wote hali zao ni mbaya na wamelazwa katika wodi namba moja na mbili, watatu hali zao ni mbaya zaidi zaidi wapo kwenye uangalizi maalumu,” alisema Muuguzi Mkuu
wa hospitali hiyo, Dkt. Thomas Isdory.
Alisema wamepokea mwili wa mtu mmoja mwanaume ambaye tiketi aliyokutwa nayo ilisomeka kwa jina la Joshua anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30.
Aliwataja majeruhi waliolazwa hospitalini hapo kuwa ni Said Omar, William Claud, Jesse Joseph, Eliah, Ambakisye, Josia Chonga, Godi Sanga, Nasra Nyagawa, Jane Mligo na wawili ambao bado majina yao bado hayajafahamika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment