27 November 2012

Watu watatu wafariki katika matukio tofauti



Na Lilian Justice, Morogoro

WATU watatu wamefariki dunia katika matukio tofauti mkoani Morogoro, likiwemo la mwanafunzi wa darasa la saba katika
shule ya Msingi Maguha, iliyopo wilayani Kilosa, Rina Gidion
(7), kugongwa na gari.


Kamanda wa Polisi mkoani humo, Faustine  Shilogile, alisema ajali hiyo ilitokea Novemba 24 mwaka huu, saa 3 asubuhi katika eneo la Maguha, wilayani humo.

Alisema gari lenye namba za usajili T 995 BSK, aina ya Toyota Duet, iliyokuwa ikiendeshwa na Bw. Ahombile Kapyela (35), ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Dar es Salaam.

Kamanda Shilogile alisema Bw. Kapyela alikuwa akitokea mkoani Dodoma kwenda Dar es Salaam ambapo alipofika eneo la Maguha alimgonga mwanafunzi huyo na kufariki dunia papo hapo.

“Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu zake ambapo mtuhumiwana anashikiliwa na polisi na chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa gari lake,” alisema.

Katika tukio jingine, mwendesha pikipiki aliyefgahamika kwa jina la Brayton Musa (20), mkazi wa Kigwasa, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari katika eneo la Gwata, Barabara ya Kinonko wilayani Morogoro.

Kamanda Shilogile alisema ajali hiyo ilitokea Novemba 24 mwaka huu, saa moja asubuhi katika eneo hilo.

Alisema pikipiki hiyo ilikuwa na namba za usajili T 605 BUE, aina ya  Fekon iliyokuwa ikiendeshwa na marehemu ikitokea Kinonko kwenda Gwata, lakini ilipoteza mwelekeo, kuanguka na kusababisha kifo chake hapo hapo. Chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa pikipiki.

Wakati huo huo, mkazi wa Tandai ambaye ni mkulima aliyefahamika kwa jina la Faustine Francis (55), amekutwa
akiwa amejinyonga kwa kutumia shuka juu ya mti wa
mshelisheli hatua tano kutoka nyumbani kwake.

Tukio hilo limetokea katia eneo la Tandai, wilayani Morogoro ambapo sababu iliyochangia achukue uamuzi huo haijafahamika.

No comments:

Post a Comment