27 November 2012

Wanaume watano mbaroni wakidaiwa kuuza miili yao


Zubeda Mazunde na Angelina Faustine

JESHI la Polisi mkoani Ilala, linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kufanya biashara ya kuuza miili yao.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Marietha Komba, alisema watu hao walikamatwa juzi, saa tano asubuhi katika eneo ya Buguruni Chama, jijini Dar es Salaam.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika msako mkali wa polisi na kukutwa wakiuza miili yao kinyume cha sheria.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Sadam Hussen (17), Ramadhani Haji (35), Mathias Machumu (22), Joseph Salum (36) na Jawe Mgaya (35) wote wakazi wa Dar es Salaam.

Wakati huo huo, Kamanda Komba alisema mwanaume mmoja jina lake halijafahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 45-50, amekufa katika mazingira ya kutatanisha.

Alisema tukio hilo limetokea juzi saa saba mchana katika eneo la Vingunguti ambapo marehemu aliishiwa nguvu ghafla na kuamua kupumzika chini ya mti, kuanza kutapika damu na kufariki dunia.

Kamanda Komba alisema chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment