29 November 2012

VETA yaanika madhara ya ukosefu wa mitajiNa Willbroad Mathias

TATIZO la ukosefu wa mitaji kwa vijana wanaohitimu Vyuo vya Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA) limeelezwa kuwa ndicho chanzo cha vijana hao kushindwa kujiajiri.

Hayo yalisema jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi VETA, Leha Lukindo, wakati wa semina ya siku moja kwa wadau mbalimbali wa sekta hiyo, iliyoandaliwa na VETA ili kujadili masuala mbalimbali yakayosaidia kuboresha mafunzo yanayotolewa na vyuo hivyo.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa vijana wengi wanaohitimu katika vyuo hivyo wana ujuzi wa kutosha lakini mitaji ya kufungua shughuli zao ndiyo kikwazo.

"Kwa ujumla kwa sasa soko la ajira limebaki katika sekta binafsi, na vijana wengi wanaohitimu kwetu
wanakuwa na ujuzi wa kutosha lakini mitaji ndiyo kikwazo,"alisema Lukindo.

Akizungumzia kuhusu lengo la semina hiyo,mkurugenzi huyo alisema kuwa wao kama VETA wana wajibu wa kuhakikisha elimu inayotolewa na vyuo walivyovisajili  siyo tu kwamba viwasaidie  wahitimu kujiajiri ama kuhajiriwa bali iwaweke katika mazingira ya ushindani wa kupata ajira kimataifa na ndiyo maana wakaamua kukutana na wadau kutafuta mbinu mbadala.

Alisema kuwa hadi sasa VETA imeshasajili zaidi ya vyuo 500 hivyo inawajibu wa kuhakikisha inavisimamia na kuvijengea mfumo mzuri wa kutoa mafunzo bora.


No comments:

Post a Comment