29 November 2012

Tanzania yapongezwa kutoa elimu ya chanjo


Na Jesca Kileo

TANZANIA imepongezwa kwa matumizi mazuri ya chanjo na elimu wanayoitoa kwa wanawake kuhusu umuhimu wa chanjo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano na wao wenyewe.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linaloshughulika na mambo ya usambazaji wa chanjo duniani(GAV)Bi.Emilly Blitz alisema Tanzania inaongoza kwa Afrika kwa matumizi mazuri ya chanjo kwa asilimia 90.

Bi.Emilly alisema licha ya pongezi hizo kwa kushirikiana na mashirika mengine duniani kama vile (UNICEF) wameandaa mkutano mkubwa utakaofanyika Afrika kwa mara ya kwanza na utafanyikia Tanzania.

Pia alisema kuwa itakuwa ni mara ya kwanza duniani kote kuruhusu waandishi wa habari kushiriki,lakini pia kuna vipengele hawataruhusiwa kushiriki kwakuchangia mada.

Alisema mkutano huo utawakutanisha wadau kutoka mashirika mbalimbali pamoja na viongozi wakubwa kutoka nchi mbalimbali duniani lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya chanjo zinazotolewa.

"Tutawakutanisha viongozi wakubwa wa nchi mbalimbali pamoja na wadau wengine kutoka mashirika tofauti duniani ili tuelezane umuhimu wa matumizi ya chanjo pamoja na namna ya kuzitumia,"alisema Bi.Emilly.


No comments:

Post a Comment