30 November 2012
UBADHIRIFU WA BILIONI 86/- Mnyika ambana William Ngeleja *Adai wizi huo ulitokea akiwa Waziri wa Nishati *Amtaka Muhongo asiwe muoga wa kujibu hoja
Na Daud Magesa, Mwanza
MBUNGE wa Ubungo Bw. John Mnyika, amesema aliyekuwa Waziri wa Nishati, Bw. William Ngeleja, hawezi kukwepa ukiukwaji wa sheria katika manunuzi ya mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme wa dharura.
Alisema kutokana na hali hiyo, upo umuhimu wa Serikali kumfanyia uchunguzi kwani wakati ukiukwaji huo unafanyika, Bw. Ngeleja alikuwa Waziri wa Wizara hiyo.
Bw. Mnyika aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Sahara, Wilaya ya Nyamagana,
jijini Mwanza na kuongeza kuwa, ubadhirifu huo umesababisha
kero kwa wananchi kutokana na umeme kukatika mara kwa mara.
Alisema umefika wakati wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, anapaswa kuwaeleza Watanzania msimamo wa Wizara yake kuhusu ubadhirifu huo.
“Waziri Muhongo ameukuta unadhirifu huu ambao ulifanywa kipindi ambacho Bw. Ngeleja akiwa Waziri wa Wizara hii, asitumie kivuli cha utaalamu alionao kutomiza majukumu yake ya Uwaziri kwani nafasi aliyonayo ni ya kisera si kitaaluma,” alisema Bw. Mnyika na kudai kuwa sakata hilo ni moja kati ya mengi.
Alisema Kampuni ya Aston Power, ilipeleka mitambo ya kufua umeme Nyakato, jijini Mwanza lakini hivi sasa haijulikani ilipo
wala mitambo yake mbali ya kulipwa fedha ya walipa kodi
lakini bado imeshindwa kuzalisha umeme.
Aliongeza kuwa, Kambi ya Upinzani bungeni, aliliomba Bunge kuunda tume ya kufanya uchunguzi wa kijinai kuhusu matumizi
fedha za ununuzi wa mafuta ya kufua umeme wa dharura.
Bw. Mnyika alisema Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), alifanya uchunguuzi maalum wa kawaida na
kubaini ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ya mafuta.
“Nililiomba Bunge limruhusu CAG afanye uchunguzi wa kijinai wakati wa hotuba yangu kama Waziri Kivuri wa Nishati, Julai 2011 kuhusu suala umeme wa dharura,.
“CAG akafanya uchunguzi wa kawaida na kubaini ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ya umma lakini taarifa hiyo haikuwekwa wazi hadi sasa,” alisema Mnyika na kuoongeza;
“Mwaka 2012, umeibuka ufisadi mwingine ambapo kauli ya Bw. Muhongo kuwa Waziri hawezi kujibu lolote kuhusu taarifa za CAG, akidai hataki malumbano si sahihi,” alisema.
Alisema umefika wakati Prof. Muhongo, kusema alichokikuta wizarani hapo kama sehemu ya kutimiza majukumu yake ya
Uwaziri asiwe muoga wa kujibu hoja na kukwepa majukumu yake.
“Nimsaidie katika hatua ya sasa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, Bw. Ngeleja anatakiwa kuchungunzwa kutokana na uzembe wake na kuisababishia hasara kubwa serikali.
“Hayo yametokea akiwa Waziri, ukiona msomi anakimbia hoja ujue kuna hoja ya msingi, Prof. Muhongo asimame na kusema, nitawataja wengi nitakaporejea Dar es Salaam na kutoa nyaraka za siri pia nitaeleza na masuala mengine ya ziada,” alisema.
Alisema haya yanayoendelea kutokea sasa ni uzembe wa Serikali, ingawa vyombo vyake vinafahamu ufisadi huo ndiyo maana alilitaka Bunge liunde tume ya kuchunguza mzunguko wa fedha za ununuzi wa mafuta katika kampuni ya Carmel, Puma na Oryx.
Alisema Bunge lilishindwa kuwajibika na ufisadi huo ambao ni sehemu ya mtandao mpana kati ya watendaji wa Wizara, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), na sekta zingine ambapo mpango wa umeme wa dharura ni kichaka cha kuchuma fedha za walipa kodi.
Majira lilipomtafuta Bw. Ngeleja ili kujibu madai hayo simu yake ilikuwa imezimwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SI VEMA KUMLAUMU WAZIRI KWANI MAAMUZI MENGI HUFANYIKA KATIKA MSINGI WA" COLLECTIVE RESISPONSIBILLITY" NA RAIS AKIWA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAWAZIRI NI UPEO FINYU KUMLAUMU WAZIRI IWAPO HAKUNA SEHEMU INAYOONYESHA ANA UWEZO WA KUSHINIKIZA MAAMUZI
ReplyDeleteWW mwenye upeo hujui Waziri ni Mwakilishi wa Rais? Kumlaumu Waziri ni sawa na kuilamu serikali inayoongozwa na baraza la mawaziri Rais akiwa Mwenyekiti wao. Sasa tatizo ni lipi?
DeleteAU wewe tuambie alaumiwe nani katika hili?