27 November 2012
Polisi kufanya mandamana ya kupinga ukatili wa kijinsia
Jesca Kileo na David John
JESHI la Polisi nchini, leo litafanya maandamano ya kwanza tangu lianzishwe ili kupinga ukatili wa kijinsi kwa watoto na wanawake.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia na kusisitiza kuwa, wameamua kufanya hivyo kutokan na ongezeko la vitendo vya ukatili nchini.
Alisema ukatili wa kijinsia umekithiri katika maeneo mengi
nchini hivyo kusababisha amani ya nchi kupotea.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Bi. Angellah Kairuki, alisema ukatili wa kijinsia unakwamisha maendeleo ya nchi kwa kiasi kikubwa hivyo kila mmoja anapaswa kupambana nao kwa kutoa elimu katika jamii.
Alisema vitendo hivyo vimekuwa vikifanyika muda mrefu na kuifanya jamii iamini kuwa ukatili huo ni sehemu ya maisha yao ambapo utafiti uliofanywa mwaka 2010 na idara ya twakimu, ulibaini asilimia 39 ya wanaume wanaamini unyumba ni
sehemu ya haki yao.
“Vitendo vya ukatilio vinakatiliwa katika amri 10 za Mungu na kwenye vitabu vyote vya dini hivyo wanawake hawapaswi kupigwa bali wanahitaji kulindwa na kuheshimiwa,” alisema Bi. Kairuki.
Aliongeza kuwa, changamoto kubwa iliyopo ili kufikia malengo hayo ni kutoa elimu ili kila jamii iweze kuelewa haki za binadamu na sera ya Taifa ya 2009 ya kuwalinda watoto na wanawake.
Hata hivyo, Bi. Kairuki alisema baada ya siku 16 za kupinga ukatili huo, anaamini jamii itawajibika kukomesha ukatili huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment