27 November 2012

Akosa sh. 7,700 kwa kushindwa kumaliza ndizi 70, akwamia 40


Na  Patrick Mabula, Kahama

KATIKA hali isiyo ya kawaida, mkazi wa Mjini Kahama, mkoani Shinyanga, Bw. Seleman Hamis (27), juzi aliwashangaza wakazi
wa huo baada ya kutamba kumaliza ndizi mbivu 77 lakini alipofika ya 40, alichemsha na kujikuta katika wakati mgumu.


Tukio hilo lilitokea katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi mjini
humo baada ya Bw. Hamis, kuahidiwa sh. 7,700 kama atakula
ndizo hizo na kuzimaliza bila kupumzika.

Shuhuda wa tukio hilo, Bw. Fabian Benjamin, alisema kijana huyo alipingana na mtu mmoja (jina linahifadhiwa), na kudai yeye ana uwezo wa kula ndizi hizo ambazo kila moja ilinunuliwa sh. 100.

Alisema ubushi huo ulikusanya kundi kubwa la watu waliotaka kushuhudia tukio hilo ambapo Bw. Hamis alipofika ndizi ya 10, alifanya mazoezi ya kukimbia umbari mfupi na aliporudi
aliendelea na kazi aliyopewa.

“Alipofika ndizi ya 30, kasi ya ulaji ilianza kupungua, baada ya kula ndizi ya 40, alijikuta katika wakati mgumu na kudai tumbo lake limejaa hivyo alisalimu amri na kukosa sh. 7,700 alizoahidiwa.

“Huyu Bw. Hamis anafanya kazi ya kuosha magari, siku za nyuma aliwahi kupinga na mtu mwimgine na kufanikiwa kula chapati 20 pamoja na soda sita lakini kwenye ndizi amechemsha.



No comments:

Post a Comment