21 November 2012

Padre: Jitokezeni kushiriki mikutano ya katiba Temeke



Na Andrew Ignas

WITO umetolewa kwa waumini wa Kanisa Katoliki, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, kujitokeza katika mikutano ya hadhara inayoandaliwa na Tume ya Kukusanya maoni ya Katiba Mpya.

Padre wa kanisa hilo, Benedict Shayo alitoa wito huo mwishoni mwa wiki baada ya misa takatifu iliyofanyika kwenye kigambo
cha Mikoroshini kilichopo ndani ya Parokia ya Chang'ombe.

Alisema umefika wakati wa waumini wa kanisa hilo kupinga ndoa ya jinsia moja isiweze kuingizwa kwenye katiba na kusisitiza kuwa, katiba Waitakayo Watanzania ni ile ambayo itachochea maendeleo yao na kukuza uchumi wao si kubariki ndoa hizo.

Aliongeza kuwa, Watanzania wanapaswa kutoa maoni ya kutungwa sheria maalumu ambayo itawachukulia hatua wanawake waanaotoa mimba kwa masusudi pamoja na kufungwa jela.

“Tusipokuwa makini, suala la utoaji mimba makusudi linaweza kuwepo katika kipingele cha katiba yetu kwa madai ya kupanga uzazi jambo ambalo ni dhambi kubwa kwa Mungu,” alisema.

No comments:

Post a Comment