19 November 2012

Jitihada zaidi zinahitajika kumaliza utapiamlo nchiniNa Rachel Balama

TANZANIA imetajwa kuwa miongoni mwa nchi 21 za Afrika kati ya 36 duniani zilizo na asilimia 90 ya watoto wenye utapiamlo.

Pia ni miongoni mwa nchi 10 Duniani zilizoathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo kuliko katika  Bara la Afrika

Takwimu zinaonyesha kuwa watoto 47,500 walio chini ya miaka mitano, wanafariki kila mwaka kwa matatizo hayo.

Kwa mujibu wa Jarida la Panita toleo la Mei mwaka huu, watoto 47,500 walio chini ya umri wa  miaka mitano hufa kila mwaka kwa utapiamlo huku asilimia 42 ya watoto hao wakidumaa.

Jarida hilo limebainisha pia kwamba Tanzania ni moja kati ya nchi 10 zilizoathirika zaidi na utapiamlo, huku ikishika nafasi ya tatu barani Afrika.

Ripoti ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyotolewa Aprili mwaka huu, iliutaja Mkoa wa Manyara kuongoza kwa utapiamlo nchini, huku ikielezwa kuwa katika mwaka 2010 Mikoa ya Iringa na Mbeya iliongoza kwa tatizo hilo.

Tatizo la utapiamlo limeenea maeneo mengi nchini kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo hali mbaya ya uchumi na ukosefu wa elimu ya lishe.

Watoto 43,000 nchini, wapo katika hatari ya kupoteza maisha mwaka huu, kutokana na kukosa vyakula vyenye virutubisho vinavyohitajika kujenga mfumo imara wa kinga za mwili.

Kwa mujibu wa utafiti wa Uwazi-Twaweza kwa kushirikiana na Asasi za Policy Forum na Sikika, inakisiwa kuwa muongo mmoja uliopita zaidi ya watoto 600,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano wamefariki dunia nchini kutokana na utapiamlo, unaosababishwa na lishe duni.

Mtoto mwenye utapiamlo akiugua ugonjwa wa kuharisha, malaria au homa ya mapafu, anakuwa na uwezekano mkubwa wa kupoteza maisha.

Kiwango cha juu cha utapiamlo kinasababisha vifo, lakini ni mara chache sana watoto kufa kwa njaa.

Wanakufa kwa sababu lishe na vyakula vyao havina virutubisho vya msingi vinavyohitajika kujenga mfumo imara wa kinga za mwili na kuwafanya wawe na afya.

Utapiamlo unadhoofisha uchumi kwa sababu wakulima na wafanyakazi hawawezi kutoa nguvu zao zaidi, hali inayosababisha kupata hasara kwenye uchumi ambapo inakadiriwa kuwa asilimia 2.6 ya pato la taifa, hupotea.

Vifo vya watoto wenye utapiamlo vingeweza kuepukika kwa jitihada na kujituma kwa mamlaka za lishe kusimamia masuala ya lishe ipasavyo.

Hali hiyo inadhoofisha jitihada za nchi kufikia malengo ya MKUKUTA na malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG) na hivyo ni vyema hatua zikachukuliwa.

Zipo njia ambazo zinaweza kupambana na utapiamlo ikiwa ni pamoja na kuanzisha urutubishaji vyakula na unyonyeshaji kamilifu wa maziwa ya mama.

Hata hivyo kwa njia zote hizo bado Tanzania inafanya vibaya, kwani ni asilimia 13.5 tu ya watoto wachanga ndio wanaonyonya maziwa ya mama pekee kwa miezi 4-5 wanapozaliwa, wakati kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani watoto wanapaswa kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita.

Kama Tanzania ingeanzisha urutubishaji unga na mafuta ya kupikia, vifo 6,700 vya watoto vingeepukwa kila mwaka na kuleta faida ya sh bilioni 153, kwa mwaka.

Ndani ya muongo mmoja uliopita hakuna jitihada kubwa za kivitendo za kupunguza utapiamlo zilizoanzishwa hapa nchini.

Kwa kuweka viwango na kusimamia urutubishaji chakula na kuhamasisha unyonyeshaji kamilifu wa maziwa ya mama kwa watoto wanaozaliwa hadi umri wa miezi sita, kwa mujibu wa tafiti Kituo cha Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wanaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Tafiti mbalimbali zimeeleza kuwa watengeneza vyakula nchini, wameripotiwa kukwama kurutubisha vyakula kwa sababu viwango rasmi havijawekwa na mamlaka husika hali inayosababisha Tanzania kuwa nchi ya tatu barani Afrika iliyoathiriwa na utapiamlo.

Makundi ya misaada ya kibinadamu yanaonya kuwa kupanda kwa bei za vyakula kunaweza kurudisha nyuma mafanikio katika kupambana na tatizo la njaa.

Mashirika ya chakula ya Umoja wa Mataifa yameeleza kuwa watu milioni 868 walikabiliwa na uhaba wa chakula kati ya mwaka 2010 hadi 2012 kiwango ambacho ni sawa na asilimia 12.5 ya idadi ya watu wote duniani.

Takwimu mpya zinaonyesha kuwa jumla ya watu milioni 925 walikabiliwa na uhaba wa chakula mwaka 2010 na mwaka 2009 walikuwa watu bilioni 1.02.

Ripoti mpya ya benki kuu ya dunia huonya kwamba utapiamlo unagharimu nchi za maskini kama asilimia 3 ya GDP yao wa kila mwaka, wakati watoto wenye utapiamlo wanadhima kwa kupoteza zaidi ya asilimia 10 ya kupata uwezo wa maisha yao.

Ripoti hiyo imeweka wazi kwamba  utapiamlo huweza kuongeza hatari za kuathiriwa na ukimwi, vilevile hupunguza idadi ya wanawake na watoto wanaweza kuepukana na malaria.

Utapiamlo umekuwa kwa muda mrefu na unapunguza kasi ya  maendeleo ya uchumi na kuendeleza umaskini.

Nchi zilizoendelea ambazo zimewekeza pesa nyingi kwenye lishe ya watoto hupata faida kubwa kwa mfujaji yao.

Athari za ukosefu wa lishe zinaonekana wakati wa ujauzito na katika kipindi cha miaka miwili ya maisha, na hasara hii ya chanzo zinazo athiri ni afya, maendeleo ya akili, busara, elimu, tija.

Nchi za Afrika na Asia kusini zimeathiriwa sana na na ukimwi kwa hiyo mafanikio ya mpango wa ukimwi katika Afrika unategemea uangalifu katika masuala ya lishe.

Kuendeleza lishi kunahitaji nguvu ya wazazi, jamaa, na nguvu ya wenyeji na kitaifa na pia huduma za umma hasa maji na usafi.

Ili kuepukana na tatizo la utapiamlo zinahitajika za nguvu  za msaada katika utafiti na utetezi, kutia moyo na kushawishi serikali kuweka  masuala ya lishie katika mipango ya nchi husika.

Aidha vyombo vya habari duniani vina jukumu kubwa la kuishawishi serikali kuangalia mambo ya lishe kwa uangalifu sana.

Pia  ni muhimu kwa viongozi kurudia hali ya kisasa ambayo  inasababisha masuala ya lishe kutokuwa na mfuko wa kutosha katika kuboresha hali hiyo kwa lengo la kutokomeza utapiamlo.

Kiasi cha dolla milioni 235  kila mwaka zinahitajika ili kutatua na kuendeleza mipango ya lishe  katika bara la Afrika.

Jitihada hizo zinahitaji makubaliano ya nchi zinazoendelea kwa  kutia mkazo juu ya masuala ya lishe.No comments:

Post a Comment