17 May 2012
KUTEMWA UWAZIRI: Maige afichua siri *Mwanasheria ajipanga kuchukua hatua *Kuanika uozo wa Maliasili bungeni
Na Salim Nyomolelo
ALIYEKUWA Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige, amefichua siri nzito zilizochangia kung'olewa katika wizara mojawapo ikiwa ni kugusa maslahi vigogo wenye nguvu kubwa na ushawishi wa hali ya juu.
Bw. Maige ilifichua siri hiyo jana kupitia ujumbe wake alioutoa kwenye mtandao wa kijamii.
Aliongeza kuwa maamuzi aliyokuwa akiyatoa wakati akiwa waziri wa wizara hiyo alijua fika kuwa hayawafurahishi vigogo hao.
"Kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu... ni ngumu kukabiliala na wabaya. Wapo waliojipanga ukiwavamia hovyo hovyo unaondoka wewe," alisema Bw. Maige na kuongeza; "Ndivyo ilivyotokea."
Alisema maamuzi yake aliyokuwa akisimamia ndiyo yamemfanya yamfike yaliyotokea. Alisema akiwa wizarani alisimamia sheria na kuwapa vitalu Watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza.
"Ni Waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records (kumbukumbu) za matukio ya mwaka 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya Maige ya 2011," alisema Bw. Maige na kuongeza;"Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi.
Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu...bado nasisisitiza hivyo."Alihoji kuwa; "NI waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai, ni waziri gani aliyeonesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Lakini mimi sikusita kuchukua hatua."
Alisema anawahakikishia wazalendo kuwa wamepoteza mpambanaji aliyejitolea kupambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi.
Bw. Maige alisema alitumia kila aina ya uwezo wake kuzawadia taifa lake utumishi uliotukuka.
Alisisitiza kuwa maamuzi hayo magumu yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. "Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda," alisema Bw. Maige akinukuu maneno aliyowahi kuyatamka Bungeni na kuongeza;"Watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini muda haukuruhusu, ila nitarudi bungeni na nitasema."
Kuhusu sakata la nyumba alisema suala hilo amelifafanua na kutoa vielelezo. "Kila mbunge aliyetaka alikopeshwa sh. milioni 290, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba," alisema.
Alisema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa Hati Wizara ya Ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB tawi la Azikiwe na Dodoma alikokopa au amtafute muuzaji.
Alisema maeneo yote hayo atapata rekodi ya bei. "Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia...mwanasheria wangu anashughulikia suala hilo," alisema Bw. Maige.
Kwa upande wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Maige alisema haikumgusa, kwani ilikuwa inaishia Juni 2010, wakati yeye alipewa dhamana ya kuongoza wizara hiyo Novemba 2010.
Kuhusu biashara ya wanyamahai, Bw. Maige alisema hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wa uongozi wake mwaka 2011 na kuwa matukio ya utoroshaji yalipobainika, walifungua mashitaka kwa watuhumiwa na kufunga biashara hiyo.
Aliahidi kuwawakilisha wananchi wa Jimbo lake la Msalala kwa mujibu wa katiba na ahadi zake kwao atazitekeleza hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo. Bw. Maige kabla ya kuteuliwa kuwa waziri kamili wa wizara hiyo mwaka 2010, alikuwa naibu waziri akiwa chini ya Bi. Shamsa Mwangunga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hongera sana Maige Mb, najua unachapa kazi na ni mzalendo ila ni chuki binafsi na kama ulivyosema umegusa maslahi binafsi ya watu...wazalendo tunasubiri useme yote bungeni ili akina Lembeli na wenzake waone kuwa walikuonea tu... labda Lembeli alitarajia uwaziri kwa kusema uwongo? mbona yeye alifanyakazi huko maliasili na kufanya ufisadi mbona hatusemi anadhani hatujui.....
ReplyDeleteAndika nini alikifanya mhe lembeli ili wasomaji wafahamu, si busara kuzusha jamani
DeleteKwa nn mtu akitimuliwa ndo aanze kujikosha? kwani ulizaliwa ili udumu kuwa waziri au kiongozi? Adui yu kokote
Huku ni kutapatapa tu. Alikuwa wapi kuyasema hayo mpaka anaachwa kwenye uwaziri ndio aseme? Hakuna lolote bora akae kimya tutamwelewa. Huo uozo auseme na awataje hao "WAKUBWA" vinginevyo akae kimya.
ReplyDeletemaige acha unafiki, kama unataka kuwa shujaa mbele ya watz taja hao wezi wa rasilimali zetu, na kama uwezi basi kaa kimya nawe uwe mwizi. Tunakusubili jimboni 2015 kukuangusha. Wewe na magamba wenzio nyote hamna kitu. CCM ndo ilikupa ulaji na ndo hiyo imekunyanganya, kama umechukia vua gamba.
Deletemfa maji haachi kutapatapa
ReplyDeleteMaige kuwa na busara zaidi ya hapo. Huakuna sababu ya kusema leo hii umewagusa vigogo ndo umeondolewa uwaziri. Kwa nini hukuwa wazi kwa kila kitu ili hali ukijua hatari iliyokuwa inakukabili?. Amua kuwa mkweli kwenye kikao kijacho - si kwa lengo la kurejeshe uwaziri wako, la hasha, ni kujaribu kuweka rekodi sawa tuu. Huna haja hata kidogo ya kuka na jambo moyoni. Siasa za nchi hii zimeharibiwa kabis na CCM. Ukiwa muazi sisi tuko tayari kukupokea na tukakupa ubunge kwa tiketi ya chama chetu -- BUT WE NEED TO KNOW THE TRUTH.
ReplyDeleteMAIGE, NAKUPA POLE. KOSA KUBWA AMBALO VIJANA WENGI KAMA WEWE WANAFANYA MPAKA LEO, NI KWENDA CCM ILI KUPATA MADARAKA. NI VIZURI UMEJUA HAYO, KWAMBA MAKADA HAWAPO KWA AJILI YA WANANCHI, WAMEKENGEUKA HAO, NA HAKUNA NAMNA YOYOTE YA KUWABADILI ZAIDI YA KUWANG'OA, NA KUWANG'OA PEKEE KULIKOBAKIA NI KWA KUPITIA CHAMA MAKINI NA KINACHOJALI MASLAHI YA WATANZANIA, NA CHENYE MACHUNGU NA NCHI. KAZI KWAKO, UKIPIGANA UKO HUKOHUKO UJUE UNAJITAFUTIA KIAMA. H A M A !
ReplyDeleteMJINGA SA MAIGE
ReplyDeleteMAIGE UMESUBIRI WAMEMWAGA UNGA NDO UNATAKA KUMWAGA MBOGA.KWANINI UNAKUWA NA KIGUGUMUMIZI KUWATAJA HAO VIGOGO.ACHA KUJIFANYA KONDOO KWENYE NGOZI YA FISI.2015 UNAPIGWA CHINI AU VUA GAMBA UVAE GWANDA.
ReplyDeletemume kula sana nchi hii huu ndio mwisho wenu.kwanini hao vigogo ulishindwa kuwataja kabla ya wabunge hawaja jenga hoja bungeni kuusu wizara yako.TANZANIAN ARE TIRED TO HEAR THOSE STORIES WHAT THEY NEED THEY WANT CHARGES.OUR NATURAL RESOURCES ARE BEING MISUSED BECAUSE OF POOR MINISTERS LIKE YOU.
ReplyDeleteRASHID YASIN KWEYUNGA
ECKERNFORDE TANGA UNIVERSITY
maige ni mdanganyifu.......!! tena inaonekana ana degree ya kudanaganya....!! mbona enzi za utawala wake hakusema hayo yote....???. jipange kwanza mjomba halafu uje kumake headlines. huu siyo wakati wake kaka. ulipewa nafasi lakini ukamuaibisha aliyekuteua kushikilia nafasi hiyo...
ReplyDeleteWhat goes around comes around.That is the
ReplyDeleteprice of your deeds.You better shut up your
BIG mouth.
Mimi simuelewi Bwana Maige,anaposema hayo anajikomba CCM, au anaisaliti? ye yuko wapi sasa? anajua yaliyomkuta Mwakyembe? hayuko makini hafai kuwa hata balozi wa nyumba kumi hiyo ni trela tu, kama hakufundwa atavundikwa. BONGO FIRST
ReplyDeletemaige pole bwana ndo ukubwa
ReplyDeletenampa pole sama Maige,avue gamba avae gwanda
ReplyDeletegwanda ndo kitu gani yote gamba na gwanda ni ujinga mtupu
DeleteMIMI SISHANGAI KWA SERIKALI YA CCM, YAPO MAMBO MENGI SANA UKIWA NDANI HUNA UHURU WA KUYASEMA UKISHATOKA NDO! MTU UNAONGEA SASA KWA BWANA MAIGE TUNATAKA UONGEE UKIWA NDANI YA CCM, TUNASUBIRI BOMU BILA WOGA INGAWA NASHAURI UKILIPUA TAYARI KIMBIA MAANA USIPOANGALIA UTALIPULIWA WEWE.
ReplyDeleteThe statement made by Maige does not make anything but rediculous.This is just the sample of the wrotten regime.
ReplyDeleteAma Kweli mfa maji haachi kutapatapa. Maige unapoteza muda wako na nadhani unazidi kujipalia mkaa mbele ya wenzako wa CCM. Bora ukae kimya umalizie muda wako vizuri kwani wavaa gwanda tayari watachukua jimbo lako ifikapo 2015
ReplyDeletemaige inaonekana inakuhuma sana kupigwa chini unajizalilisha mwenyewe
ReplyDeleteTATIZO LA NCHI ZA ULIMWENGU WA TATU NI KUINGIA KWENYE DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI BILA KUULIZA ABC ZAKE KAMA VILE TULIVYOVAMIA UTNDAWAZI BILA MAANDALIZI BUNGE LA KWANZA LA KIPINDI CHA RAIS KIKWETE LILIONDOA ILE DHANA YA WABUNGE KUKAA KAMA KAMATI YA CHAMA MIJADALA IKAWA NI KUSHAMBULIANA SERIKALI NA ILE YA UPINZANI IKAWA SI RAHISI KUIONA TENA FUJO TU WABUNGE NA MAWAZIRI KUSHAMBULIANA SIAMINI KUNA MAAMUZI YA WAZIRI PEKE YAKE LAZIMA YAWEPO MAAMUZI YA PAMOJA YA MAWAZIRI MAAMUZI NA WABUNGE WAKE
ReplyDeleteMaige nakushauri uhamie chadema maana unakata tawi la mti ambalo umelikalia likikatika utaumia.
ReplyDeleteMaana hatukuelewi lengo lako ni nini kutufahamisha hayo leo sisi wananchi hatuna uwezo wa kukurudishia uwaziri nenda ukamlilie aliyekupa.Kamsaidie kamanda lema kusongesha mbele m4c.
hebu soma hii meseji ''Kwa upande wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Maige alisema haikumgusa, kwani ilikuwa inaishia Juni 2010, wakati yeye alipewa dhamana ya kuongoza wizara hiyo Novemba 2010.'' jamani yeye si alikuwa naibu waziri wa wizara hiyo??????? kichekesho
ReplyDeleteKaka Maige yote unayoyasema ni kweli,wizara nzito sana na kuingilia maslahi ya mafisadi ndo mshara wake huo, wengi tulipitia huko na hata kuitwa si watanzania lakini siku zao zinahesabika. Tutarudia siasa za 1967 ili wanyonge wapate sauti...Wamekuwa walafi kama kila wakionacho wataka kiwe chao
ReplyDeleteNAPATA WASIWASI NA UKOMAVU WA KISIASA NA UZALENDO WA MAIGE. JE ULITAKA UACHWE UHARIBU MPAKA LINI? JE, HUONI KUWA RAIS ALIKOSEA KUKUPA UWAZIRI? WEWE UNGEFUNGA DOMO LAKO, UKAE KIMYA USUBIRI KUSHTAKIWA. MBONA HIYO CPA HAIKUSAIDII KUCHANGANUA MAMBO? UNATUTIA SHAKA SISI WASOMI. SASA TUTAANZA KUHOJI SIO TU UHALALI WA MALI ZAKO, LAKINI PIA UHALALI WA VYETI VYAKO. ISIJE IKAWA ULINUNUA, NA NDIO, MAANA UNALILIA UWAZIRI. POLE SANA!!!!!!!!!!!!!
ReplyDelete