*Apigwa mawe, mapanga na wananchi
*Saba wauawa, watatu familia moja
Na Moses Mabula, Tabora
ASKARI Polisi mwenye namba E 9530, PC Joseph wa Kituo cha Kidogo cha Polisi cha Puge, Wilaya ya Nzega ameuawa kwa
kupigwa mawe na kukatwa mapanga na wananchi wakati akiwa katika kazi ya kukamata watu wanaolima bangi katika Kijiji cha Mwakashanshara Tarafa ya Puge .
Pia wananchi hao walimjeruhi askari mwingine mwenye namba G 246 ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Bw. Liberatus Barlaw alisema tukio hilo limetokea saa nne asubuhi katika kata hiyo.
Bw. Barlaw alisema kwa sasa hana zaidi la kuzungumuza kuhusu tukio hilo hadi hapo taarifa kamili ya jeshi hilo itakapokamilika na kutolewa kwa vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka katika kata hiyo, chanzo askari huyo aliuawa wakati wakifanya operesheni maalumu ya kukamata bangi na wanaolima zao hilo.
Vyanzo hivyo kwa nyakati tofauti vililiambia Majira kuwa askari hao walikuwa watano katika oparesheni hiyo.Moja ya vyanzo hivyo vilisema kuwa wananchi hao waliwakamata askari wawili na kuwapiga lakini wengine walifanikiwa kukimbia.
Chanzo hicho kilisema kuwa askari hao hawakuwa na silaha za kutosha katika oparesheni hiyo hali iliyofanya wananchi hao kuwadhibiti kirahisi na kusababisha kifo na mmoja wao na kumjeruhi na mwingine ambaye amelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Ndala iliyopo katika tarafa hiyo.
Inadaiwa kuwa wananchi katika taarafa hiyo wamekuwa na uhusiano mbaya na askari wa kituo hicho kutokana na kile kinachodaiwa polisi kuwanyanyasa raia kwa kuwakamata mara kwa mara bila sababu ya msingi.
Wakizungumza na Majira baadhi ya askari polisi wilayani hapa kwa nyakati tofauti walisema vitendo hivyo vya kuuawa kwa askari vimekuwa vinatokea mara kwa mara hasa wananchi wakiwa na kinyongo na baadhi ya askari.
Moja ya askari ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema kuwa sasa kila mwezi matukio hayo yamekuwa yakitokea katika Kanda ya Magharibi jambo linalowafanya wahofie usalama wa maisha yao.
Alisema kuwa kuna haja sasa kwa serikali kutoa elimu kwa wananchi hasa katika kanda hiyo ambao wamekuwa wakitumia zaidi Kikosi cha Sungusungu kuwauwa raia bila kuwapeleka katika na vyombo vya kisheria.
Wakati huo huo Juddy Ngonyani kutoka Sumbawanga anaripoti kuwa watu watatu wa familia moja wakazi wa Kijiji cha Miombo kilichopo katika Kata ya Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa wameuawa na miili yao kuchomwa moto baada ya kushambuliwa na kundi la wananchi kijiji hicho kwa kile kilichodaiwa walihusika katika kifo cha mtoto miaka minne katika kijiji hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Bw. Isunto Manatge aliwaambia waaandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku baada ya kundi la wananchi hao kuvamia nyumba ya Luciano Chole (62) na kuwashambulia wanafamilia hao kwa zana mbalimbali za jadi na kusababisha mauti yao.
Kamanda Mantage aliwataja wanafamilia waliouawa kuwa ni Luciano Chole (62) na mkewe, Adelina Mulele (54) na mtoto wao Jailos Silvanus (29).
Akifafanua juu ya tukio hilo Kamanda Mantage alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa siku tatu kabla ya tukio hilo mtoto mwenye umri wa miaka minne aliyefahamika kwa jina la Geminus Kwimba alitoweka nyumbani kwao katika mazingira ya kutatanisha na siku iliyofuata mwili wa mtoto huyo ulikutwa umetupwa kwenye dimbi la maji.
Alisema baada ya tukio hilo wakazi wa kijiji hicho walihisi kuwa mtoto huyo ameuawa na Jailos Silvanus hivyo kuvamia familia hiyo.
Kamanda Mantage alisema kuwa usiku wa kuamkia juzi kundi la wananchi hao lilivamia nyumba ya wanafamilia hao na kumshambulia Jailos ambapo wazazi wake waliamua kuingilia kati kwa lengo la kumuokoa lakini nao walishambuliwa hadi kufa na miili yao kuchomwa moto.
Hata hivyo mara baada ya kufanya unyama huo watu hao walikimbia na bado wanatafutwa na jeshi hilo.
Katika tukio jingine Kamanda Mantage alisema kuwa jeshi hilo linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Bi. Anna Kasubi (80) mkazi wa Kitongoji cha Kitupa kilichopo katika Kijiji cha Majimoto Kata ya Mamba Tarafa ya Mpimbwe wilayani Mpanda.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mashala Mashige(28) pamoja na mkewe aitwae Luca Kasamya(25) ambao ni majirani wa marehemu huyo.Kamanda Mantage alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana ingawa kinasadikika kuwa kinatokana na imani za kishirikina.
Tunakoelekea Watanzania kwakweli ni kubaya sana. Tumwombe Mungu atunusuru na kadhia hii. hali hii siyo yenyewe jamani!!
ReplyDelete...kama kulikuwa na mahusiano mabaya baina ya polisi na raia je kwanini polisi hao walitumwa kwenda huko wakiwa wachache na wasio na silaha? (mkuu wa kituo aulizwe.
ReplyDeleteBangi ni tatizo la muda mrefu hapo kulikuwa na ulazima wa kukamatwa siku hiyo? je wasingeweza kutathmini hatari kabla ya kufanya hivyo au kuomba operation maalum toka kwa kamanda wa mkoa?
Polisi tumieni SARA model (Scan-identify the problem,Anayse,respond and assess)
Ninachokiona hapa polisi wanajua tatizo (scan)lakini wakaruka hatua ya analyze (Tathmini) na kwenda ukamataji (respond) Na ndio maana hayo yote yametokea.Maana wangefanya tathmini sahihi wasingetuma askari hao wachache na bila silaha,maana tahtmini yao ingewaonyesha wanahitaji operation ya askari wengi kwasababu pia mahusiano yao raia sio mazuri.
Katika hatua ya assessment tuanona kuwa lazima itafutwe mbinu mbadala na sio kama hiyo iliyotumika.Je polisi jamii iko wapi hapa?
Wewe mtoa mada wa 12.52 ni afisa wa usalama nini, mana umeongea kwa ufasaha sana, hongera hiyo ndo uchangiaji unaotakiwa...hata hivyo wananchi waliohusika wachukuliwe hatua kali, nashauri polisi ifanye oeresheni maalum eneo hilo ili wakamatwe na kuwa mfano, hata kama ni kijiji chote,viongozi wa kijiji pia lazima wanajua nao waadhibiwe.
ReplyDeletePoleni wanafamilia mliofiwa.Lakini mimi nashangaa serikali ambayo imeshindwa kukamata wafanyabiashara wanaoingiza madawa ya kulevya toka nchi za asia na wanatajirika badala yake mnatuma polisi kwenda kutafuta wanaolima bangi nzega.Naomba wahusika waliangalie sana swala hili.Uchumi ni mgumu kwa wananchi ndiyo maana wanalima bangi.Kwanza zao la bangi ni kiungo cha mboga kama ilivyo ufuta.
ReplyDeleteNi kweli polisi hawakujitayarisha. Poor intelligence ndio ilioharibu operesheni yao. Polisi lazima mujipange operesheni kama hizi.
ReplyDeleteKuhusu tukio hili, sheria itumike vema katika kutafuta ukweli, sio kukandamiza au kulipa kisasi kwa wana kijiji.
...Nakubaliana kabisa na mchangiaji wa SARA Model yaani (Scan,Analyse,Respond and Assess).Aidha nakubaliana na uchangiaji wa mtoa maoni ya poor intelligence ambayo pia yamemezwa na SARA model ukiangalia kwa makini.
ReplyDeleteNi kwanini tusihalishe ukulima wa bangi nchini?Maana vilevile kuna mashamba mengi tu tarime,arumeru Aruha na sehemu nyinginezo?
Watuhumiwa watafutwe na wafikishwe mahakamani ili haki itendeke.ukweli utafutwe maana unaweza kukuta polisi wenyewe walienda kutafuta chochote (walijituma kazi) mkuu hana taarifa.Na kama ndivyo mkuu ataruka kimanga ili kujiondoa kwenye hilo tatizo.
Pole jeshi la polisi wote.pole mtanzania,pole familia.
Operesheni kama hiyo ya kukabiliana na bangi, madawa ya kulevya n.k uongozi wa kitongoji au kijiji vinapaswa kuhusishwa kwa karibu ili kupata taarifa za kiintelejensia na kuweka mataarisho muhimu.
ReplyDeleteKule Tegeta, DSM mabaunsa walienda bila kushirikisha viongozi wa kitongoji na madhara yake tuliyaona. Pia Polisi msitegemee sana kuwa kwa vile tuna bunduki mnaweza kuzuka maeneo bila kushirikisha viongozi wa maeneo husika.
Hili ni somo kwa POLISI na hata wale wenye hela ambao hutegemea ukubwa wao kutaka kutekeleza operesheni ambazo zinaweza kuwa hatarishi.
Mdau
James Bond.
SARA model,Poor intelligence na kushirikisha uongozi wa kitongoji au kijiji ni muhimu kwa operation zozote za kipolisi.Hayo ni mawazo muhimu kabisa ya kuchukua.
ReplyDeletePOLENI SANA POLISI.
ReplyDeleteNDUGU ZANGU MIMI NINACHOONA TATIZO HILO NI LA POLISI NAOMBA WAANDISHI WA HABARI WAKAMUULIZE MKUU WA POLISI TANZANIA KWA NINI WANANCHI WANAPIGA POLISI?
1-KUNA UHUSIANO WA POLISI KUPEWA PESA NA WAUZA BANGI AU GONGO KWA HIYO NI MRADI WA POLISI KILA WAKATI KWENDA KUKINGA BAKULI KUPEWA PESA IKTOKEA TU MUUZA BANGI AKISEMA SINA PESA LEO POLISI WANAKUJA KUMKAMATA.
2-JE HILO TATIZO MKUU WA POLISI HALIFAHAMU AU CHA MUHIMU NI POLISI MKUU WA POLISI ATUME AU AENDE YEYE MWENYEWE AKAWAULIZE WANANCHI WA PALE WATAMUELEZA MENGI YANAYOFANYWA NA POLISI,SIO HAYO TU NI MENGI.NDUGU WANANCHI TUTAFUTE CHANZO NA HIYO NDIO DALILI YA TANZANIA HATUNA AMANI TUTAKUJA KUONA POLISI WANAUAWA WANAOISHI MITAANI USWAHILINI KWA SABABU ZA UZURUMAJI WAO HUU KWA WANANCHI
Nakubaliana na ykweli kwamba polisi ndio wenye jukumu la kuzuia makosa na kufanya ukamataji pindi wanapopata taarifa za uhalifu.Kama walipata taarifa za mashamba ya bangi tayari yaliyolimwa je walishindawaje kupata taarifa za uandaaji wa mashamba hayo au upandaji wake??!
ReplyDeleteOperation yao inaonyesha imehusisha askari 5 na hawana bunduki wakati huohuo tunaambiwa kuwa mahusiano yao na raia wa eneo sio mazuri kwahiyo walitakiwa kuangalia viashiria vya usalama (threats) au kwa jambo lolote lisilo la kawaida kutokea katika operation yao ambapo wangeweza aidha kuahirisha operation au kuomba waongezewe nguvu na kamanda wa mkoa au polisi wilaya.
Haingii akilini kama lilikuwa ni jambo tu la kwenda kufanya operation walitakiwa kukusanya habari zaidi za kiitelejensia ili kufahamu wamiliki,masoko yao na wakati ambapo wamiliki wanakuwepo kwenye mashamba yao.Au hata wahusika wangeweza kukamatwa kwa ushirikiano na wahusika wa vijiji,au kata kwa ushirikiano mzuri tu bila kuleta bugudha kama hiyo na maisha ya watu kupotea.
Kama kulishaonekana kuwa uhusiano wa polisi na raia wa eneo sio mzuri kwahiyo kwenda kufanya ukamataji ilikuwa ni kama kuongeza chumvi kwenye kidonda.Kuna ubaya tayari,ukamatji uliongeza ubaya zaidi.
bdo turudi kwenye SARA Model:
Scan (tambua tatizo)
Analysis (kusanya habari zaidi kuhus tatizo kwa upana,angalia ukubwa wa tatizo kwa jamii na je wananchi wanalisemaje hilo katika eneo lao)
Repond (chukua hatua baada kupata habari kamili katika utendaji wa polisi ikiwa pamoja na kuangalia viashiria vya uslama wao,na mahusiano yao na jamii inayowazunguka.
Assessment (je hatua walizochukua zimesaidia kuondoa tatizo? au zimeongeza tatizo.Hii itawasidia nini hakikuwasidia katika hatua zao waizochukua na pengine kubadili mbinu ya upambanaji na tatzio lenyewe.
Udhaifu mkubwa amabo polisi wameonyesha ni kutofahamu kukusanya habari za uhalifu.Wao walikurupuka na matatizo ya kukurupka matokeo yake ndio hayo Think slownly and act quickly'.Haya mashamba ya bangi hayakuwa dharura ambayo yalihitaji maamuzi ya dharura.
Inauma sana kwa askari kuawa kwa mazingira ambayo ukamataji au maamuzi yake yangekuwa bila madhara.
Jambo jingine ni kwamba polisi wetu wanaonekana kuwa wakukimbizana na matukio (reactive) na sio proactive (kuzuia zaidi)kwanini wasingeshughulikia swala hili kabla ya kupanda??
Vyovyote itakavyokuwa waliohusika na maujai wakamatwe na raia wafundishwe kuheshimu vyombo vya usalama na wakati huohuo polisi wetu liwe fundisho kwa yaliyotokea.
Poleni watanzania.
SARA MODEL UPO MAKINI, ILA SHAKA YANGU NI KWAMBA ENDAPO POLISI WANGEWASHIRIKISHA VIONGOZI WA KIJIJI JUU YA HABARI YA KUKAMATWA KWA WALIMAJI WA BANGI,TAARIFA INGEWAFIKIA WAHUSIKA KWA SABABU NI SEHEMU YA WANAKIJIJI PIA POLISI WAACHE KUFANYA KAZI KWA MAZOEA,POLENI WAFIWA
ReplyDeletePoleni sana wana usalama wa raia kwa msukosuko mliopambana nao,
ReplyDeleteKi kweli ni kwamba polisi wetu hufanya kazi kitemi zaidi ya maalifa yaliyo wapeleka pale moshi.
Kuna biashara ambazo dunia huwa haziitaji kukurupuka tuu kuwa leo tunaenda kukamata,Bangi,Madawa ya kulevya kienyeji tuu,laa hapana.
Biashara hii ni ya pesa tamu (sweet money) na huwa ina channel ndefu sana,kwani yule aliyekuwa pale kijijini si mtumiaji wa mwisho,sasa basi ili kufanya swala hili au watu hawa wa chain nzima kuhusishwa ni swala linalohitaji muda,kwa maana ya upelelezi ambao huwa hauchukui siku moja wala mwezi mmoja,kwanza ni lazima uwatambue wahusika,kwa picha ambazo zilipigwa na maafisa upelelezi,kisha mienendo yao ya kila siku,ushahidi wa maeneo ya matukio,mabadilishano ya bangi kwa pesa,Msafirishaji wa hiyo bangi,huwa inaelekea wapi mara ikitokea hapo,Mara nyingi biashara hizi huusisha wanasiasa wakubwa,matajiri,na hata wakubwa wa vitengo vya usalama.
Uchunguzi ukishakamilika,afisa upelelezi huipitia ripoti na kuiwasilisha kwa mkuu wa polisi na kwa kushirikiana na wapelelzi huandaa timu ya kuwakamata wote hawa wahusika kwa siku moja bila kufanya makosa.
Na baadae wahukumiwe kwa vifungu na ibara za sheria.
Si muafaka nyinyi polisi wa kawaida kuonyesha sura zenu huko kila wakati kwa ajili ya vijisenti tuu.
Tanzania ni nchi yenye sifa yake duniani,tuilinde heshima yetu, Aibu sana kwa mkuu wa jeshi la polisi.
Asanteni kwa uwanja huu
TATIZO KUBWA NA JESHI LETU LA POLISI LA SASA; NGUVU ZOTE ZA INTELIJENSIA ZIMEWEKEZWA KWENYE SIASA CHAFU NA KUACHA MAJUKUMU YAO. TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA....
ReplyDeleteTheoretically, intelligence ndio msingi mkuu wa kazi za Polisi duniani. SARA Model, if its practiced at all in Tz, becomes activated once 'useful' intelligence is available.
ReplyDeleteZipo other factors kama vile conditions that precede and accompany the problem, capability of the Unit in question, resources available, training, backup/support unit(s), ,strengths and limitations of adopted response to the target, etc
Ni kweli lazima jeshi letu lijipange vizuri kabla ya kuvamia matukio ya uhalifu.
Haya maoni yanasomwa na hawa jamaa au.(local bobbies)-police wetu.
ReplyDeleteMaoni yaliyotolewa hapa na baadhi ya wachangiaji ni mazuri hatakuliko kufikiri kwa polisi wetu.
Waambieni wachkukue maoni hayo ni muhimu kwa kesho.
Vita ya wauza madawa ya kulevya,heroine,cocein,bangi nk ni ngumu na hatari. Polisi wasifanye jambo rahisi wanapokwenda kuwakamata watu hawa inabidi wajitayarishe.humu katika watoa maoni kuna wavuta bangi,sasa hata maoni yao yako hovyohovyo tu
ReplyDelete